TRA

TRA

Friday, March 3, 2017

MARUFUKU KUSAFIRISHA MCHANGA WENYE MADINI NJE YA NCHI: RAIS MAGUFULI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi na wafanyakazi wa  kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo wilayani Mkuranga, Pwani, Machi 2, 2017.(PICHA NA
FRANK SHIJA – MAELEZO).


NA BENJAMIN SAWE, MKURANGA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli amezuia usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda kuuchenjua nje ya nchi akitaka shughuli hizo zifanyike nchini.
Akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vigae cha Tanzania Goodwill Ceramic Rais, Magufuli alisema uchenjuaji wa mchanga wa madini nje ya nchi kunaikosesha Serikali mapato ikiwa ni pamoja na wizi madini hayo.
”Ndio maana nilikataa kusaini mkataba wa EPA kwa sababu kupitia mkataba huo, ni vigumu kwa kampuni za Tanzania kushinda zabuni katika nchi za Ulaya lakini ni rahisi kwa kampuni za Ulaya kushinda zabuni Tanzania kutokana na kukomaa kiteknolojia, na hata zinaposhindanishwa kampuni za Tanzania na Ulaya ni rahisi kwa kampuni za Ulaya kushinda, jambo litakalochangia kuua kampuni zetu”alisema Rais Magufuli.
Alisema Tanzania ni mwananchama wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC hivyo kujengwa kwa kiwanda hicho kutapelekea kiwanda hicho kunufaika kiuchumi.
Rais Magufuli alisema kwa muda mrefu wawekezaji wamekuwa wakisafirisha malighafi za Tanzania nje ya nchi kwa ajili ya uzalishaji na kupelekea wananchi kutumia bidhaa zisizo na ubora.
Katika uwekaji wa jiwe la msingi wa Kiwanda hicho Mheshimiwa Magufuli alisema imefika wakati kwa Tanzania kuuza bidhaa zinazozalishwa viwandani na kuachana na kusafirisha malighafi nje ya nchi kwa ajili ya uzalishaji.
Katika hatua nyingine Rais John Pombe amesema Serikali yake haina chakula cha kuwapa wananchi wanaopatwa na tatizo la njaa badala yake amewataka wananchi kufanyakazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula cha kutosha.
Awali akitoa salamu zake kwa Mheshimiwa Rais, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Adelhelm Meru amesema kujengwa kwa kiwanda hicho ni faida kwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Nae Balozi wa Tanzania nchini Mhe. Lu Youqing alisema Serikali ya China kwa sasa iko katika mkakati wa kuhamishia viwanda vyake vingi barani Afrika na imeamua kuichagua Tanzania kuwa moja kati ya nchi watakazohamishia viwanda hivyo kutokana na kuridhishwa na dhamira inayoonyeshwa na serikali katika kuleta maendeleo.
Alisema China inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika harakati za kujikomboa hivyo itaendelea kuiunga mkono kuhakikisha inafikia uchumi mzuri.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani leo.Kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd Fang Habibi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru(wapili kushoto).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akimsikiliza kwa makini Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd, Robin Huang (kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho leo Wilayani, Mkuranga. Katikati ni Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho jina lake halikupatikana.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger