Mshambuliaji aliyewajeruhi watu tisa kwa shoka katika mji wa
Düsseldorf amepelekwa kwenye hospitali ya wagonjwa wa akili. Msemaji wa
idara ya waendesha mashtaka wa serikali ameeleza kwamba mtu huyo
amepelekwa hospitali badala ya kuwekwa kizuizini baada ya hakimu
kukubali maombi ya kuchukuliwa hatua hiyo. Mshambuliaji huyo mwenye umri
wa miaka 36 raia wa Kosovo alibainika kuwa na matatizo ya akili. Mapema
wiki hii aliwajeruhi watu tisa kwenye kituo cha treni cha mji wa
Düsseldorf uliopo Kaskazini Magharibi mwa Ujerumani. Polisi wamesema
kutokana na matatizo ya kiakili huenda mtu huyo alitarajia polisi
wangempiga risasi na kumuua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment