Wapinzani wa rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Park
Geun-hye wanashinikiza kiongozi huyo akamatwe siku moja baada ya
mahakama kuamuru kiongozi huyo aondolewe madarakani. Wakati huo huo mtu
wa tatu amepoteza maisha yake kutokana na maandamano yaliyoanzishwa
baada ya kutangazwa habari za kiongozi huyo kuwa ni lazima ajiuzulu.
Mwandamanaji huyo mfuasi wa rais Park aliyekuwa na umri wa miaka 74
aliyejulikana kwa jina moja Lee alipoteza fahamu katika malumbano na
polisi hapo jana. Kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la Yonhap
Lee alifariki mapema leo katika hospitali moja ya mjini Seoul. Hata
hivyo kilichosababisha kifo chake bado hakijajulikana. Park Guen-hye
mwenye umri wa miaka 65 na rais wa kwanza mwanamke wa Korea kusini
alivuliwa mamlaka na bunge tangu mwezi Desemba mwaka uliopita kutokana
na kushirikiana na rafiki yake Choi Soon Sil katika kuzilamisha kampuni
kadhaa kutoa fedha na kumruhusu mshirika wake huyo kujiingiza katika
maswala ya serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment