Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto)
akiangalia eneo kutakapojengwa kituo cha kupooza na kusambaza umeme,
Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua vituo
vya kupooza na kusambaza umeme jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni
wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO).
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara jijini
Dar es Salaam ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vipya vya kupooza
na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini pamoja na kukagua eneo
kutakapojengwa kituo cha Kupooza umeme katika eneo la Kigamboni.
Baada
ya ukaguzi huo Dkt. Kalemani alieleza kuridhishwa kwake na kasi ya
ujenzi wa vituo hivyo. Hata hivyo aliwaagiza watendaji wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na mkandarasi, kuhakikisha kuwa ujenzi
huo unakamilika mwishoni mwa mwezi wa Aprili mwaka huu ili wakazi wa
Mbagala, Kurasini, Kigamboni na maeneo ya jirani wapate umeme wa uhakika
usiokatika mara kwa mara.
Aidha
aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa, wanaweka uzio katika
eneo kutapojengwa kituo cha kupooza umeme cha Kigamboni ili lisiingiliwe
na wavamizi na hivyo kukwamisha juhudi za Serikali za kupeleka umeme wa
uhakika kwa wananchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment