Watuhumiwa
wa kesi ya uhujumu uchumi Miss Tanzania wa Zamani Shose Sinare na
kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya n Sioi Sumari wakiwa katika
kizimba cha mahakama ya kimu mkazi kisutu mara baada ya kusomewa
mashtaka yanayowakabili
Kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya na Sioi Sumari
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani
ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna
Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.
Hayo
yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.
Mbali na
Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi
Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa
fedha wa kiasi cha USD milioni sita.
Baada ya
taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba
mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na
siyo kuleta liugha za ujanja ujanja.
“Tunaomba
upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za
ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la
kutueleza umekamilika ndaniya nchi lakini nje bado, haileti maana
yoyote.”Amesema Magafu.
Akijibu
hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani
umekamilina inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi Fulani hivyo
ameugiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko nje
ikoje.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.
Mbali na
shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma
za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.
Wanadaiwa
kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba
2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania
kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.
aliyekuwa Miss Tanzania Shose Sinare akishuka katika ngazi za mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
SHARE
No comments:
Post a Comment