Viongozi wakuu wa Kiislamu na Kikiristo kutoka kanda ya Mashariki ya
Kati wanakutana leo kwa siku ya pili katika mji mkuuu wa Misri-Cairo kwa
mkutano unaojadili kuimarisha utangamano wakati ambapo mizozo
inayochochewa na tofauti za makundi ya kidini yakiikumba kanda
hiyo.Mkutano huo kwa jina uhuru na uraia ulioanza jana unaongozwa na Al
Azhar mojawapo ya taasisi kubwa za Kisunni iliyo na makao yake Cairo.
Kiongozi wa Al Azhar Sheikh Ahmed Tayeb amesema kuziondoa lawamani dini
dhidi ya kuhusishwa na ugaidi ni suala lisilotosheleza tena katika
wakati huu ambapo kuna changamoto za kikatili. Sheikh Tayeb amesema
makundi kama ya Dola la Kiislamu IS yanatafsiri visivyo dini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment