Malaysia leo imewafungulia mashitaka wanawake wawili wanaotuhumiwa
kumuua kaka yake kiongozi wa Korea Kaskazini kwa kutumia kemikali
inayoathiri mfumo wa neva mwilini na kuua dakika chache baadaye. Siti
Aisha raia wa Indonesia mwenye umri wa miaka 25 na Doan Thi Huong raia
wa Vietnam mwenye umri wa miaka 28 huenda wakanyongwa iwapo watakutwa na
hatia ya kumuua Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kuala Lumpur mnamo tarehe 13 mwezi Februari.Polisi waliwafikisha
wanawake hao wawili mahakamani wakiwa wamevishwa pingu na kuvalishwa
fulana za kuzuia risasi. Kim Jong Nam alifariki baada ya wanawake hao
kumpaka usoni kemikali ijulikanayo VX, ambayo Umoja wa Mataifa umeitaja
kama silaha ya maangamizi makubwa. Korea Kusini na Marekani zimesema
mauaji hayo yalipangwa na Korea Kaskazini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment