Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa taarifa ya
shirika hilo kwa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakati kamati
hiyo ilipotembelea miradi ya shirika hilo iliyopo jijini Dar es salaam,
Kamati hiyo imesifu kazi zinazofanywa na shirika hilo kutokana na
kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya kuuza na
kupangisha.
Mh.
Haji Mponda Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
akizungumza na Mama Blandina Nyoni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Shirika la Nyumba la Taifa NHC
Mkurugenzi
wa Ubunifu shirika la nyumba la NHC Bw. Issack Peter akitoa maelezo kwa
wajumbe wa kamati ya bunge ya Hesabu za serikali wakati waliptembelea
miradi ya shirika hilo inayojengwa jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na waandishi
wa habari wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ilipotembelea
miradi ya shirika hilo.
Wajumbe wa Kamti ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakitembelea mradi wa 711 unaotekelezwa na shirika hilo uliopo Kawe
Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa maelezo kwa wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ilipotembelea kwenye miradi
hiyo.
Mkurugenzi
wa Fedha NHC Bw. Felix Maagi akizungumza na mmoja wa wajumbe wa kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali waliotembelea katika miradi ya NHC.
Wajumbe
wa Kamti hiyo Munde Tabwe kushoto na mama Burra wakijadiliana jambo
wakati kamati hiyo ilipotembelea katika miradi ya shirika hilo jijini
Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba Mama Blandina Nyoni
akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu
na mkurugenzi wa Ubunifu Isaack Peter.
Isaack
Peter Mkurugenzi wa Ubunifu NHC akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali wakati walipotembelea miradi ya shirika
hilo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Kamti ya Bunge ya Hesabu za serikali Mh. Haji Mponda akiuliza swali
kwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati
wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea katika miradi ya shirika hilo
jana.
SHARE
No comments:
Post a Comment