Mkutano
Mkuu wa mwaka wa 26 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
wakiwa kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
Arusha, (AICC), leo Machi 23, 2017. Kauli mbiu ya mwaka huu ya mkutano
huo ni, "“Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (pichani juu), ameupongeza
Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutekeleza kwa vitendo Mpango wa pili wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa
nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye
uwekezaji wa viwanda..
Waziri
ametoa pongezi hizo leo Machi 23, 2017 wakati akifungua Mkutano wa 26
wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye ukumbi
wa Simba wa KItuo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini
Arusha.
“Nimeelezwa
kuwa nyinyi PPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF) pamoja na Jeshi la Magereza mmeingia kwenye makubaliano ya pamoja
ya kuanzisha viwanda vikubwa na vya kisasa vya kuzalisha sukari katika
eneo la Mkulazi na Mbigiri Morogoro.” Alisema Waziri Dkt. Mpango
Akifafanua
zaidi kuhusu mpango wa PPF kwa ushirikiano na NSSF na Jeshi la Magereza
kwenye uwekezaji mkubwa wa viwanda, Dkt. Mpango alisema, “Mimi na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na
Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama ni mashuhuda wa hilo
kwani tuliweza kujionea eneo la mradi la Mkulazi na ujenzi wa
miundombinu tulipolitmbelea katika eneo hilo mwezi Desemba mwaka jana.”
Alisema.
Akitoa
hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini ya PPF, Bw.Ramadhan Khijjah, (pichani juu), alisema, kauli
mbiu ya mkutano huu wa 26 wa Wanachama na Wdau wa PPF ni “Tanzania ya
Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Hifadhi ya Jamii”.
“PPF
imedhamiria kwa dhati kabisa kuunga mkono dhamira ya Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ya kjuifanya
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda kama inavyoelezwa
katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/2017 hadi
2010/21.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio alisema Mkutano wa mwaka huu
ni wa siku mbili na umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 800 na lengo la
kuchagua kauli mbiyo iliyoelezwa hapo juu ya “Tanzania ya Viwanda;
Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii” ili kukuza uelewa wa
Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa
Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia
kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua
wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.
Mkurugenzi wa Fedha wa PPF, Bw. Rmmanuel Martin, akitoa taarifa ya fedha ya Mfuko
|
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi.Irine Isaka, (mbele kushoto), ni miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria mkutano huo
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizunhumza na Meneja wa PPF, Mkoani Arusha, Bw. Sule
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw.Adam Mayingu (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Bw. Daudi Msangi
Meneja
Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), akijadiliana jambo na
Meneja Kiongozi, Uandikishaji wanachama na Elimu, Mbarouk Magawa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akitoa hotuba ya ukaribisho
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa PPF
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka WCF
Wajumbe wakiwa mkutanoni
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba yake ya ufunguzi
Bi.Stephanie Nandi, akiwa na mwanaye mchanga akitoa ushuhuda baada ya kufaidika na Fao la Uzazi
Mfugaji
Bw.Mrida Mshoto Marocho, akitoa ushuhuda kuhusu faida aliyopata ya bima
ya Afya, baada ya kujiunga na mpango wa Wote Scheme
Bw.Kulwa
Mohammed, mmoja wa watu waliotoa ushuhuda wa jinsi alivyofaidika na Fao
la Elimu. Kulwa ni Mwanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM)
Mjumbe akipitia jarida la PPF lenye maelezo ya kina kuhusu shughuli mbalimbali za Mfuko
Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Bw. Steven Alfred akitoa maelezo ya uwekezaji ya Mfuko huo.
|
Waziri
wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, akimkabidhi tuzo, Kaimu Meneja Mwandamizi
Rasilimali Watu wa TANESCO, Nathan K. Daimon, baada ya Shirika hilo la
Umeme nchini kuwa mshindi wa jumla kwa Mashirika ya Umma yanayowasilisha
michango yao kwa wakati na mingi inayofikia Bilioni 2 kwa mwaka.
Waziri
wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu, (kushoto), akipeana mikono na Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, wakati akimkabidhi vifaa vya
hospitali kwa niapa ya PPF pembezoni mwa mkutano huo. PPF imetoa msaada
wa vifaa hivyo vyenye thamani inayokaribia Milioni 100. Vifaa hivyo kwa
mujibu wa Waziri Ummy, vitapelekwa kwenye vituo vya afya 11 kote nchini
|
Waziri Ummy akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo
|
Mgeni
rasmi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kushoto),
akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (katikati),
na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Hifadhi ya Jamii,
(SSRA), Bi.Irine Isaka, wakati akiondoka ukumbi wa Simba baada ya
kufungua mkutano huo
|
SHARE
No comments:
Post a Comment