Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke amesema nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika kutoa mafunzo maalum ya Menejimenti ya Maafa kwa wataalamu wetu.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ofisini kwake mjini Dodoma.
Akielezea
lengo la ziara hiyo, Balozi Cooke alisema Serikali yake inataka kuiunga
mkono Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inajipanga kukabili na
kurejesha hali pindi yanapotokea maafa.
“Masuala
ya maafa yapo nchi nyingi ikiwemo kwetu Uingereza ingawa mafuriko na
ajali za moto zimekuwa zikiikumbaa nchi yetu mara kadhaa.”Alisema
Balozi.
Aliongeza
kuwa, Serikali ya Uingereza imevutiwa na juhudi zinazofanywa na
Serikali ya Tanzania katika kukabili na kurejesha hali ikiwa pamoja na
kuwasaidia wananchi na mali zao pindi yanapotokea maafa.
Kwa
upande wake, Waziri Mhagama alimpongeza Balozi huyo kuona umuhimu wa
kuja Tanzania na kuonesha nia ya kuisaidia nchi kwa namna mbalimbali.
“Nishukuru
kipekee kwa ujio wako na kuona umuhimu wa kuunga mkono jitihada za
Serikali ya Tanzania katika maswala mazima ya maafa na kumhakikishia
kuwa Tanzania ipo tayari na itajiandaa kuwaunga mkono kwa utayari wa
kuisaidia nchi”Alisema waziri Mhagama.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akisalimiana na Balozi wa Uingereza Nchini
Mhe.Sarah Cooke alipomtembelea waziri Ofisini kwake Bungeni Dodoma
Balozi
wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke akiongea jambo na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akiteta jambo na Balozi wa Uingereza Nchini
Mhe.Sarah Cooke alimtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.
SHARE
No comments:
Post a Comment