Msanii nyota wa
filamu Tanzania, Kajala Masanja, kulia akishiriki katika droo ya kwanza ya
bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku inayoendeshwa na Kampuni ya Biko ambapo
ilimpata mshindi wake wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambaye ni Christopher Mgaya,
Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
nchini, Juhudi Ngolo.
‘Nguvu ya Buku’
yampatia Sh Milioni 10 Christopher Mgaya
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
DROO ya kwanza
ya kuwania Sh Milioni 10 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki imempatia donge nono
mkazi wa Temeke, Christopher Mgaya na kuweka historia ya kuwa mtu wa kwanza
kujinyakulia kitita hicho kutoka kwa mchezo wa bahati nasibu wa Biko.
Droo hiyo
ilichezeshwa na msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja
akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo.
Mwakilishi
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo kushoto
akichezesha droo kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, ambapo mkazi wa
Temeke, Christopher Mgaya aliibuka na kitita hicho. Kulia ni msanii wa
filamu, Kajala Masanja, akishuhudia.
Akizungumza
katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba jumla
ya washindi 2000 walipatikana katika zawadi mbalimbali, huku Mgaya yeye
akiibuka kinara wa Sh Milioni 10.
Heaven alisema
kwamba baada ya kupatikana kwa mteja huyo, taratibu za kumkabidhi hundi yake ya
Sh Milioni 10 unaweka ili mteja huyo apate fedha zake haraka iwezekanavyo.
“Tumeanza vizuri
kwa kufanikiwa kumpata mshindi wetu wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambapo alicheza
bahati nasibu yetu, huku yeye akifanikiwa kuibuka mshindi.
Droo hiyo ya kutafuta mshindi wa Sh Milioni 10 inaendelea
Droo inaendelea kutafuta mtu wa kunyakua Sh Milioni 10
Msanii Kajala Masanja akimpigia simu mshindi wa Sh Milioni 10, Christopher Mgaya jana jijini Dar es Salaam.
“Utaratibu ni
ule ule kwasababu kila mtu anaweza kushinda kwa kuinguza muamala kwa Tigo Pesa,
M-Pesa na Airtel Money ambapo ataingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050
kwenye kipengele cha lipa bili, huku pia akiingiza namba ya 2456 kama namba ya
kumbukumbu ambapo Sh 1000 atakayocheza itampatia tiketi mbili za kushinda hapo
hapo au tiketi ya kumuingiza kwenye droo ya kuwania Sh Milioni 10”, Alisema
Heaven.
Naye Mwakilishi
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo alisema kwamba wameikagua
kampuni ya Biko na kuvutiwa na utaratbu wa mchezo wao, hali inayoonyesha kwamba
Watanzania wapo salama katika kucheza mchezo huo.
“Nimekuwa
mwakilishi wa kwanza kutoka Bodi kusimamia wakati wa kumtafuta mshindi wa Sh
Milioni 10 ambapo naamini Watanzania wataamua kucheza zaidi,” Alisema Ngolo.
Naye Mgaya
mshindi wa bahati nasibu hiyo ya Sh Milioni 10 alisema haamini kwamba ameshinda
Sh Milioni 10 hadi hapo atakapokabidhiwa kitita chake ingawa kimemfanya avuje
jasho wakati anatangazwa yeye ndio mshindi.
“Nimefurahishwa kushinda
kwangu mshiko wa Biko wa Sh Milioni 10 ambapo siamini kama nimeshinda zawadi
hiyo kubwa kutoka kwenye Kampuni ya biko,” Alisema Mgaya.
Kwa mujibu wa
Biko, mbali na ushindi wa Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na
Sh Milioni Moja zinazolipwa kila siku na papo kwa hapo kwenye simu za wateja,
ushindi wa Sh Milioni 10 utapatikana kila mwisho wa wiki kwa kuchezesha droo
inayokutanisha washiriki wote wa siku za wiki.
SHARE
No comments:
Post a Comment