Mahakama yazuia kwa muda amri ya Trump ya kusafiri
Mahakama nchini Marekani amesitisha kwa muda amri ya rais ya kuzuia
raia na wahamiaji kutoka nchi saba zenye idadi kubwa ya waislamu kuingia
nchini humo. Ikulu ya Marekani imeita hatua hiyo kuwa ni ya hatari kwa
kusema agizo hilo lililenga kuimarisha hali ya usalama wa ndani ya nchi
hiyo. Jaji James Robart ametoa amri hiyo jana Ijumaa itakayohusisha nchi
nzima. Mwanasheria mkuu wa jimbo la Washington Bob Ferguson,
aliyewasilisha pingamizi mahakamani pamoja na Jimbo la Minnesota, amedai
kwamba amri hiyo ya Rais haikufuata mchakato wa kisheria kwa wakazi
halali wa Marekani. Amri hiyo ya mahakama pia inazuia kusimamishwa kwa
mpango wa Marekani kuhusu wakimbizi ambao umeacha maelfu wakikosa
mwelekeo baada ya kupata kibali cha makazi mapya. Hatua hiyo imekuwa ni
ushindi mkubwa kwa majimbo ya Washington na Minnesota yaliyoipinga hatua
hiyo ya Trump.
No comments:
Post a Comment