Mkuu
wa Wilaya Morogoro, Regina Chonjo (wa pili kushoto) akikabidhi kwa
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo (wa tatu kulia)
sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama
pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya
wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa
ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa
wiki. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Doris Mollel, Doris W. Mollel, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Morogoro,
Dkt. Ritha Liamue, Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe na
kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John.
Mkuu
wa Wilaya Morogoro, Regina Chonjo (wa pili kushoto) akizungumza jambo
na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel (wa pili
kulia), baada ya kupokea msaada ya vitanda vitatu vya kujifungulia
wakinamama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa
kabla ya wakati "Njiti" kupumua, Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni
mwa wiki katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Wengine pichani ni Kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo (kulia), Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ritha Liamue (kushoto), pamoja na
Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe ambao ndio waliofadhili
upatikanaji wa vifaa hiyo.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Doris Mollel, Doris W. Mollel pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CBA,
Solomon Kawishe wakipanda mti katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro, baada ya kukabidhi sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya
kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto
wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi
ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel kwa pamoja na Meneja
Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe wakimsikiliza mmoja wa
wakinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati "Njiti" katika Hospitali
ya Mkoa wa Morogoro, walipotembelea wadi hiyo kutoa zawadi za Sikukuu
ya Pasaka kwa wakinamama hao, baada ya kukabidhi sehemu ya vifaa tiba
(vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za
kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua),
vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA
kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa wiki.
SHARE
No comments:
Post a Comment