TRA

TRA

Saturday, April 1, 2017

Maduro na sakata la mahakama Venezuela

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
SERIKALI  nchini Venezuela imetoa mwito kwa mahakama ya juu zaidi nchini humo kurejelea maamuzi yake iliyoyatoa wiki hii ya kufuta bunge linaloongozwa na upinzani, hatua ambayo wakosoaji wameilaani na kuiita kuwa ni mapinduzi na ya kidikteta. 

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesema katika hotuba yake ya usiku wa jana iliyorushwa kupitia kituo cha televisheni cha serikali kwamba uhasama kati ya mahakama hiyo na bunge umekwishadhibitiwa, ingawa hakutoa maelezo zaidi. 

Ikiwa tayari imefuta baadhi ya hatua za bunge tangu upinzani ulipoanza kuongoza bunge mwaka 2015 mahakama hiyo inayomtii Maduro Jumatano hii ilisema inachukua majukumu ya bunge kutokana na hatua yake ya kudharau sheria. 

 Hatua hiyo imeibua miito ya kimataifa kulaani kitendo hicho na maandamano katika mji wa Caracas. Katika hatua ambayo ni nadra hapo jana mwanasheria mkuu wa serikali ambaye pia ni mshirika wa muda mrefu wa Maduro na mwenye ushawishi mkubwa Luisa Ortega alikemea hatua hiyo ya mahakama.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger