Mwenyekiti
wa Baraza la Mawaziri wa Bonde la Ziwa Victoria ambaye pia ni Waziri wa
Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi cheti cha
shukrani, Bi. Joyce Kasebela baada
ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwa mmoja wa wadhamini
wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa
Victoria lilimalizika jana jijini Mwanza.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi),
Dkt Leonard Chamuriho (kushoto) akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki wakishiriki Kongamano la
Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria
lililomalizika jana jijini Mwanza.
Sehemu
ya washiriki kwenye Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa
Bonde la Ziwa Victoria, lililofikia tamati jana jijini Mwanza.
Meneja
wa Kiwanja cha ndege cha Jiji la Mwanza, Bi. Esther Madale (kulia)
akiwa na Bi. Joyce Kasebele wa Kitengo cha Mazingira cha Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali katika Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa
Bonde la Ziwa Victoria. Kongamano hilo lilifanyika Jijini Mwanza.
Mwakilishi
wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa Jijini Mwanza, Bi. Dorah Michael
(kushoto) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa
Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya
Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la
Ziwa Victoria jana jijini Mwanza.
Bw.
Prenanning Pamer mkazi wa Mwanza akipata ufafanuzi wa masuala ya
mazingira ndani ya viwanja vya ndege, kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi
kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi
Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, yaliyomalizika jana jijini Mwanza.
ASP
Andrew Majaliwa (kulia) akiwa ameshika moja ya vipeperushi vya Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), baada ya kupata maelezo kuhusu
mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki
wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa
Victoria, lililomalizika jana jijini Mwanza.
SHARE
No comments:
Post a Comment