TRA

TRA

Saturday, April 1, 2017

Ujerumani yawachunguza viongozi wa juu wa kidini wa Uturuki.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
INAAMIKA kuwa waendesha mashtaka nchini Ujerumani wanamchunguza mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa mamlaka ya kidini ya nchini Uturuki ya Diyanet Halife Keskin. 

Mtandao wa vyombo vya habari wa Ujerumani jana jioni umeripoti kwamba Keskini ambaye ni kiongozi wa idara ya mambo ya kigeni wa Diyanet anadaiwa kutoa mwito kwa wanadiplomasia wa Uturuki duniani kote kukusanya taarifa za wafuasi wa sheikh mwenye utata wa dini ya Kiislamu Fethullah Gulen. 

Serikali ya Uturuki inalituhumu kundi lake kuhusika na jaribio la mapinduzi lililoshindwa la Julai mwaka jana.
 Kulingana na wachunguzi hao nyaraka zilizokuwa na mwito huo wa Diyanet zilikabidhiwa kwa mamlaka ya mji wa Karlsruhe na mtu wa ndani ya taasisi hiyo. Waraka huo pia unawataka maimamu walioko Ujerumani kuwachunguza wafuasi wa Gulen.

 Mashitaka didi yake yalifunguliwa Machi 13. Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu imethibitisha kuanza uchunguzi siku chache zilizopita, wakati ambapo tayari madai ya upelelezi dhidi ya maimamu hao yakiwa tayari yanajulikana. 

Taasisi ya kijasusi ya Uturuki pia ilikabidhi orodha ya majina 300 ya wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Gullen pamoja na anuani zao kwa taasisi ya kijasusi ya Ujerumani mnamo mwezi Februari. 

Miongoni mwa majina yaliyokabidhiwa ni Mbunge wa chama cha Social Democrat, SPD Michelle Müntefering na mbunge kutoka chama cha CDU Emine Demirbüken-Wegner. 

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo mahusiano kati ya Ujerumani na Uturuki yakiendelea kuzorota.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger