Waziri Charles Mwijage akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika Mkutano maalum kati ya Sekta hiyo na Serikali.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikutana na wadau wa Sekta Binafsi mapema wiki hii katika mkutano maalum ulioandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF).
Kutoka
kushoto ni Godfrey Simbeye, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Gotfrid
Muganda Mkurugenzi Mtendaji TCCIA, Octavian Mshiu, Makamu wa Rais TCCIA
ambao ni waandaaji wa Mkutano huo maalum baina ya Serikali na Sekta
Binafsi wakiwa na Hussein Kamote, Mkurugenzi wa Huduma na Uanachama-CTI.Lengo
la mkutano huo maalum baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ulikuwa
na lengo la kuboresha mazingira ya biashara nchini, kukuza ushirikiano
kati ya Serikali na Sekta Binafsi pamoja na kuongeza njia za kukuza
uchumi utakaochochea ya azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania
kuwa nchi ya Viwanda.
Mkutano
huo uliofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango (Treasury Square) uliongozwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji (MB) Mh. Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango
(MB), Mh. Dkt. Philip Mpango na kuhudhuriwa na wabunge, makatibu wakuu
na manaibu katibu wakuu, Kamishna wa TRA, Mwenyekiti wa TPSF Makamu wa
Rais- viwanda wa TCCIA, Mwenyekiti wa TRADEMARK EAST AFRICA,
Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali nchini na wawekezaji, viongozi wa
ACT, ATE, MOAT, TASOA pamoja na wajumbe wedau wengine wa biashara.
Makamu
wa Rais Sekta ya Viwanda TCCIA Octavian Mshiu akizungumza jambo na
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage (MB) katika
Mkutano huo.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage (MB) kushoto,
akifurahia jambo na Mwenyekiti wa TPSF Bw. Reginald Mengi kulia,
anayeshuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Philip Mpango (MB).
Mkutano
huo uliipa Serikali fursa ya kusikiliza changamoto zinazoikabili Sekta
Binafsi na kukusanya maoni ya wadau wa sekta hiyo na kuahidi kuzifanyia
kazi na kuzitatua ili kuweza kuimarisha mahusiano, umoja, mshikamano,
ushiriakiano na uaminifu baina ya sekta hizi muhimu katika uchumi wa
taifa la Tanzania.
Akizungumza
katika Mkutano huo, Waziri Mwijage aliwashukuru wadau wa Sekta Binafsi
kwa kujitokeza kwa wingi ili kuzungumza na Serikali na kuwa njia hii ya
kukutana kwa vile imeonekana kuwa njema basi itaendelea kutumika ili
kuhakikisha sekta hizi zinakutana mara kwa mara. Waziri aliahidi
kushughulikia kero zinazokabili mazingira ya biashara kama kuwepo kwa
kodi na kuahidi upunguzwaji wa kodi utitiri ambazo zimekuwa kero kwa
wafanyabiashara na pia kuweka mazingira rafiki baina ya Sekta Binafsi na
Serikali.
Kwa
upande wake Waziri Mpango alisema, “Tulipofikiria wazo hili
hatukutegemea muitikio huu na kwamba ni utaratibu muafaka na napendekeza
kwa kuanzia tuendeleze huu utaratibu na tukutane angalau mara moja
katika kila robo ya mwaka, asanteni sana. Mmeipongeza serikali na hata
mmetuelezea changamoto ambazo ni za msingi sana, mmeifanya siku hii kuwa
na thamani kubwa katika kujenga Tanzania mpya”.
Waziri Philip Mpango akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika Mkutano maalum kati ya Sekta hiyo na Serikali.
Maofisa
waandamizi wa Serikali na wadau wa Sekta Binafsi wakifatilia mazungumzo
katika Mkutano maalum baina ya Serikali na Sekta Binafsi uliofanyika
mjini Dodoma wiki hii.
SHARE
No comments:
Post a Comment