Shirika
la Anga la Etihad (EAG) limeandaa kozi maalumu kwa wahandishi na
warubani inayofahamika kama ‘Think SciencE 2017’ ili kuhamasisha taaluma
ya anga ikiwa ni sehemu ya juhudi za taifa la Abu Dhab kuwahamasisha
vijana kwenye masomo ya sayansi na teknolojia.
Tukio
la uzinduzi lilifanyika katika ukumbi wa Dubai World Trade Centre na
limeandaliwa na Taasisi ya Emirates Foundation ikiwa ni miongoni mwa
maonyesho makubwa katika ukanda huo.
Mgeni
rasmi katika maonyesho hayo, ambaye piani Mkurugenzi mtendaji wa
Emirates Foundation, alizundua maonyesho hayo kisha kutembelea ofisi za
Shirika la Anga la Etihad.
Wageni
watakaotembelea ofisi za shirika hilo watafahamu mambo mbalimbali ya
uendeshaji yanavyofanyika na watajifunza jisni ya ndege zinavyorushwa.
Marubani na watumishi wa ndege watajibu maswali mbalimbali kutoka kwa
watu wanaopenda kufahamu kuhusu masuala ya anga.
Wawakilishi
wa Kitengo cha Etihad Airways Engineering watakuwepo, wataonyesha
injini ya kisasa ya ndege ya jet, vilevile watatoa ufafanuzi masuala
yanayohusiana na ndege ya 120-plus.
Pia,
kutakuwa na picha za video zinazoonyesha shughuli mbalimbali za Shirika
la Anga la Etihad jinsi linavyojihusisha na maendeleo katika ugunduzi wa
mafuta ya ya ndege ambayo ndiyo wa kwanza katika kuyatumia kupitia
mradi wake wa Sustainable Bioenergy Reseach Consortium.
Kapteni
Salah Al Frajalla wa Shirika la Ndege la Etihad, ambaye pia ni Makamu
wa Rais wa Masuala ya Usalama na Shirika la Taifa la Kuendeleza Marubani
alisema, “Hii ni chachu ya maendeleo kwa Nchi ya Falme za Kiarbu
kutokana na kuwahamasisha vijana kujiingiza kwenye taaluma ya urubani
ambapo watakuwa na ujuzi huu.
Tunatumaini
kwamba kuwanzishwa Think Science 2017 itawavutia na kuwatia moyo vijana
wengi kuanza kujadili masuala yanayohusiana na sayansi na teknolojia.
Pia kuhimiza vijana wengine wa Nchi za Falme za Kiarabu kupenda taaluma
hii hata kutamani kujiunga na Shirika la Anga la Etihad.
Pia,
katika kuwafanya wageni wavutiwe na kuelewa zaidi kuhusu masuala
mbalimbali ya Shirika la Anga la Etihad, wageni watapata fursa ya
kushindana ili kujishindia safari moja maalumu ambapo wataweza
kutembelea na kufahamu shughuli za Shirika la Anga la Etihad
linaloongoza kwenye sekta ya anga nchini Abu Dhab.
Zawadi zitatolewa kwa kwa vijana watakaooonyesha ubunifu kwenye masula ya uhandishi wakati wa mashindano hayo.
Maonyesho
ya Think Science yalizinduliwa mwaka 2012 yakiwalenga kundi la miaka
15-35 na kuwapeleka maelfu ya wageni kila mwaka . Lengo la serikali ni
kuhamasisha ushirikianao baina ya wanasayansi na wadau wa sekta ya
saynsi na teknolojia.
SHARE
No comments:
Post a Comment