Balozi
wa Msumbiji nchini Bi Monica Patricio Clemente akizungumza na viongozi
wa TCCIA walioongozana na Makamu wa Rais-Viwanda Bw. Octavian Mshiu wa
kwanza kulia, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Gotfrid Muganda pamoja na viongozi
wa TCCIA Mtwara Bw. Swallah S. Swallah-Mwenyekiti na Muhidin Swalehe.
Mkutano
huo ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa TCCIA mwenye dhamana ya Viwanda
Bw. Octavian Mshiu akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Bw.
Gotfrid Muganda pamoja na viongozi wa TCCIA Mkoa wa Mtwara Bw. Swallah
S. Swallah ambaye ni Mwenyekiti na Bw. Muhidin Swalehe- Afisa
Mtendaji.Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa TCCIA-
Viwanda Bw. Octavian Mshiu amesema mapendekezo ambayo TCCIA imewasilisha kwa Balozi wa Msumbiji nchini yanalenga kutoa ushirikiano wa karibu kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambao utawezesha uanzishwaji wa vituo katika mkoa wa Mtwara ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na misaada ya haraka kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili.
Viwanda Bw. Octavian Mshiu amesema mapendekezo ambayo TCCIA imewasilisha kwa Balozi wa Msumbiji nchini yanalenga kutoa ushirikiano wa karibu kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambao utawezesha uanzishwaji wa vituo katika mkoa wa Mtwara ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na misaada ya haraka kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili.
Makamu
wa Rais wa TCCIA-Viwanda Bw. Octavian Mshiu akimkabidhi Balozi Monica
Clemente nyaraka maalum baada ya mkutano na Balozi huyo ofisini kwake
mapema wiki iliyopita.
Balozi
Bi. Monica Patricio Clemente amesema amefurahishwa na ugeni alioupata
wa uongozi wa TCCIA na kwamba mapendekezo chanya yaliyoletwa na TCCIA
yana nafasi sahihi na muhimu katika kuboresha ushirikiano wa
wafanyabiashara wa Mtwara na Mikoa jirani ya Msumbiji kwani mahusiano ya
aina hiyo yana nafasi kubwa ya kunufaisha jamii ya wafanyabiashara,
kuongeza pato la nchi zote mbili na pia kukuza uchumi wa maeneo husika.
Balozi
Monica ameahidi kuyafanyia kazi majadiliano na mapendekezo ya TCCIA kwa
haraka ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa mikoa inayofanya
biashara pamoja ambayo matokeo yake yataleta tija kwa maslahi ya
Tanzania na Msumbiji kwa ujumla
Viongozi
wa TCCIA wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa
Msumbiji nchini baada ya mkutano wa Balozi na uongozi wa TCCIA jijini.
Katika
mkutano huo wajumbe kutoka ubalozini humo wamesema moja ya changamoto
kubwa inayowakumba wafanyabiashara wengi ni lugha ambapo wamependekeza
pia kuwepo kwa vituo maalum ambavyo vitakuwa vikitoa elimu ya lugha kwa
wafanyabiashara hao ili kuondoa changamoto hiyo.Mwenyekiti wa TCCIA
Mtwara Bw. Swallah S. Swallah ameshukuru ubalozi wa Msumbiji kwa ukarimu
na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya wafanyabiashara wa
Cape Delgado nchini Msumbiji na Mtwara nchini Tanzania. Pia alieleza
juhudi za Chemba ya Mtwara katika kukabiliana na changamoto ya lugha na
kwamba mjini Mtwara tayari kuna kituo kikubwa cha lugha kinachofundisha
watanzania lugha mbalimbali ikiwemo Kireno ambacho sasa kinatiliwa mkazo
zaidi.
Viongozi
wa TCCIA wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa
Msumbiji nchini baada ya mkutano wa Balozi na uongozi wa TCCIA jijini.
SHARE
No comments:
Post a Comment