TRA

TRA

Tuesday, May 30, 2017

ASILIMIA 24.9 HUVUTISHWA MOSHI WA TUMBAKU KWENYE SEHEMU ZA KAZI.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


NA ALLY DAUD-WAMJW DODOMA

ASILIMIA 24.9 ya watanzania huvutishwa moshi wa tumbaku katika sehemu za kazi hivyo kuchangia kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani nyingi hapa nchini.

Hayo yamebainishwa kwenye taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu inayohusu Maadhimisho ya siku ya kutotumia tumbaku duniani.

“Hali hii isipodhibitiwa vifo vitaongezeka kufikia asilimia 80 kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na milioni 8 kwa mwaka duniani kote ifikapo 2030” iliongeza taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa katika uchunguzi uliofanywa mwaka 2013 na Wizaya ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Utafiti wa Maradhi ya Binadamu(NIMR) wakishirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ulionyesha asilimia 24.9 huvutishwa moshi wa tumbaku sehemu za kazi, asilimia 14 ya watanzania hutumia tumbaku na asilimia 17 ya watanzania hawavuti lakini wanavutishwa moshi wa tumbaku.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa tumbaku inaua watu takribani milioni 6 kila mwaka na moshi wake huua zaidi ya watu laki 6 ambao sio wavutaji wa tumbaku duniani .

Mbali na hayo Wizara ya afya imedhamiria kupiga vita matumizi ya tumbaku kwa kuhakikisha hakuna matangazo ya tumbaku kyupitia kwenye mabango barabarani,luninga,redio,sinema,au kubandikwa ukutani na kwenye magari ya matangazo.

Madhimisho ya Siku ya kutovuta Tumbaku huadhimishwa Mei 31 kila mwaka duniani kote na kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo”TUMBAKU-TISHIO KWA MAENDELEO” .

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger