TRA

TRA

Friday, May 19, 2017

Baada ya ushindi wa Mali vs Niger, Serengeti Boys inahitaji sare kwenda World Cup

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

Timu ya taifa ya Mali ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano ya AFCON U-17, baada ya suluhu yao ya kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania leo May 18 2017 wamerudi uwanji kucheza dhidi ya Niger baada ya mchezo wa Tanzania na Angola kumalizika.

Mali ambao ndio Mabingwa watetezi wameingia katika uwanja wa Stade de Amitie kutafuta ushindi ili wajiweke pazuri katika mbio za kutetea taji lao na kupata nafasi ya timu nne zitakazofuzu nusu fainali kucheza michuano ya Kombe la dunia baadae mwaka huu nchini India.

Mchezo huo wa pili wa Kundi B kati ya Mali dhidi ya Niger umemalizika kwa Mabingwa watetezi Mali kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ambayo yamefungwa na nahodha wao Mohamed Camara na Hadji Drame wakati Niger wameambulia goli moja lililofungwa na Habibou Sofiane.

Ushindi huo wa Mali unawafanya kuwa sawa kwa point na Tanzania na kuwa sawa kwa kila kitu kwa maana ya magoli ya kufunga na kufungwa, Tanzania wana pointi nne wakifunga magoli mawili na kuruhusu moja sawa na Mali wakati Mali na Angola na wenye wakisalia na pointi moja wakifanana pia kwa kila kitu, Tanzania sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa mwisho dhidi ya Niger.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger