Taarifa mpya za usiku huu kuhusu hali ya mmoja wao akiwa Hospitali ya Mercy, Sioux City IA ni kwamba Mtoto Doreen amemaliza kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na Madaktari wamesema wamefanikiwa kwa ufanisi mkubwa kupita matarajio.

Doreen akiwa Hospitali, picha na maelezo ni kutoka kwa Mbunge Lazaro Nyalandu
Mtoto Doreen amehamishwa kutoka chumba cha upasuaji na kupekewa ICU na Madaktari wamesema kwasababu hali yake imeridhisha sana, baadae leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya upasuaji na kumrudisha wodi ya watoto.
SHARE








No comments:
Post a Comment