Mgeni
Rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama
pamoja na mwakilishi wa makampuni ambayo yamefadhili shughuli ya siku ya
wauguzi kutoka Benki ya NMB,Suma Mwainunu.
Picha na Joel Maduka wa Maduka online.
Benki ya NMB Tawi la Geita limetoa fulana 360 kwenye siku ya
Wauguzi Duniani lengo likiwa ni kuendelea na Jitihada zake za kuwa karibu na
jamii.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi ambapo
Kimkoa yamefanyika Mkoani Geita ,Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya
Ziwa Bi Suma Mwainunu,amesema kuwa Benk hiyo inatambua thamani ya wauguzi na
kwamba ndio maana wameamua kushiriki kwa kufadhili fulana hizo.
“Tumejisikia Vizuri sana na hivyo kwa niaba ya NMB tumeweza
kushiriki hafla hii kwa kutoa Shilingi Milioni Tatu ambazo zimetumika Kununua
Fulana ambazo mnaona wengi Tumezivaaa wauguzi hoyeeeeee”Alisema Bi Mwainunu.
Hata hivyo Bi,Suma Ameongezea kuwa Benk ya NMB
ipo karibu na wateja na ndio
maana wameshiriki hafla hiyo pamoja na wateja wao.
Aidha Bi, Suma
ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuiamini na kutumia Huduma ambazo
zinatolewa na Benk hiyo yenye matawi mbalimbali nchi nzima na pia ametoa wito
kwa uongozi wa Mkoa kushirikisha Benki ya NMB Katika maswala
mbali mbali ya Kijamii nao wakiwa na uwezo wapo tayari kushirikiana nao.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni Rasmi Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ameishukuru Benki ya NMB kwa mchango wake
katika kufanikisha sherehe hizo.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE |
No comments:
Post a Comment