Mwanadada Diane Rwigara, (pichani), ametangaza azma
yake ya kuwania Urais nchini Nchini Rwanda katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Agosti mwaka huu.
Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu
wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita katika
mazingira ya kutatanisha .
Bi Diane mwenye umri wa miaka 35 amesema, anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.
Amesema, kuna suala la usalama mdogo
ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuwawa katika mazingira ya
kutatanisha, na kwamba huwezi kusema uko katika nchi yenye amani na
usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi.
Huyu ni Mnyarwanda wa tatu kutangaza
rasmi nia ya kutaka kugombea urais nchini Rwanda wengine wakiwa ni Bwana
Mpayimana Philippe aliyetangaza kuwa mgombea binafsi na Franck Habineza
kutoka chama cha Green.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame
SHARE
No comments:
Post a Comment