Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Alphonce Slima, akiongoza semina ya kujadili vipaumbele katika bajeti ya Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha
wa 2017/2018 iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Mdau Neofita Kunambi akizungumza wakati akichangia mada kwenye semina hiyo.
Anna Sangai akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Sadick Juma mkazi wa Mbezi Beach,
akielezea changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika
Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili.
Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matibabu ya homa ya ini ambayo dawa zake hazipatikani nchini hadi zitoke India.
Moses Benard akizungumzia wajawazito
kujinunulia vifaa vya kujifungulia na suala la dawati la ukatili wa
kijinsia kuwepo vituo vya polisi.
Mdau Dalia Kalungwana akichangia jambo.
Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
wananchi wakifuatilia kwa karibu semina hiyo.
Vijana wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wameiptia bajeti ya mwaka 2017/
2018 ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
iliyotengwa na kuomba iongezwe kwa kuzingatia ukubwa wa wizara hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika
semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP)
ya majadiliano ya kupitia bajeti hiyo ili kuona vipau mbele vyake
waliombwa iongezwe ili iweze kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye
wizara hiyo ambayo imelemewa kutokana na ukubwa wake.
Kwa mwaka wa fedha wa 2016/ 2017 wizara
hiyo ilitengewa bajeti ya sh.bilioni 845 ikilinganishwa na mwaka wa
fedha wa 2017/2018 ambayo tofauti yake sio kubwa.
Akizungumza katika semina hiyo, Neofita
Kunambi alisema katika wizara hiyo kunachangamoto kubwa bila ya
kuongezewa fedha katika bajeti yake hazitaweza kuisha.
"Bila ya kuongeza bajeti katika wizara
hii wajawazito wataendelea kujinunulia vifaa vya kujifungulia tunaomba
jambo liangaliwe kwa karibu" alisema Kunambi.
Anna Sangai alisema huduma za afya
zinapaswa kuboreshwa kuanzia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na bila
kuongezwa kwa bajeti katika wizara hiyo itakuwa ni ndoto.
Mkazi wa Mbezi Beach, Sadick Juma
alisema upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, miundombinu na ukatili wa
kijinsia ni changamoto kubwa katika wizara hiyo.
Alisema licha ya kuwepo duka la Bohari
ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili (MNH),
upatikanaji wa dawa umekuwa mgumu hivyo kuifanya Muhimbili kuwa na
majengo mazuri bila ya kuwa na dawa.
"Ukitaka kuona changamoto hata ukiwa ni
mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ugua au uwe na
mgonjwa ambaye ni mwanachama uende katika hospitali hiyo kwanza
kupokelewa tu pale mapokezi ni balaa na ukifika muda wa kutakiwa kupata
dawa utaambulia panado na kuambiwa dawa hazipo" alisema Juma.
Juma aliongeza kuwa huduma ya bure kwa
watu wenye msamaha hiyo ni ndoto kwani wagonjwa hao hawasikilizwi kabisa
jambo ambalo ni hatari.
Alisema serikali imekuwa ikijipodoa kuwa
inaboresha huduma za afya lakini hali halisi haipo hivyo akitolea mfano
kwa nchi nzima maduka ya dawa ya MSD yapo nane tu je upatikanaji wa
dawa na vifaa tiba utafikia katika kiwango cha kukidhi mahitaji alihoji
Juma.
Janeth Mawinza alisema bajeti hiyo
iangalie zaidi jinsi ya kutibu magonjwa kama ya homa ya ini ambayo
matibabu yake kwa hapa nchini hayapatikani mpaka dawa itoke nchini
India.
Moses Benard alisema ikiwa mjamzito
aliopo mjini anatakiwa kujinunulia vifaa vya kujifungulia hali ikoje kwa
yule ambaye yupo kijijjini ambaye anachangamoto ya kutokuwa na fedha na
kukimbiwa na mwenza wake hivyo akaomba Waziri wa wizara hiyo kutoa
tamko rasmi la kuwataka wajawazito kutonunua vifaa hivyo wanapokwenda
hospitali kujifungua.
Wadau wengine waliongelea jijini Dar es
Salaam maeneo mengine kama Kipunguni wilayani Ilala kukosa kuwa na
zahanati au hospitali hivyo kulazimika kwenda wilaya ya Kisarawe kupata
matibabu jambo ambali linashangaza hivyo wakaomba bajeti ya wizara hiyo
iongezwe ili kufanikisha upatikanaji wa zahanati au hospitali katika
maeneo yao.
SHARE
No comments:
Post a Comment