Chama cha soka
nchini Uingereza FA kimesema kitaanzisha sheria mpya kwa wachezaji
wanaojirusha hovyo uwanjani ama wale wanaodanganya kuumia wakati wa
mchezo ili kupoteza muda.
Robert Snodgrass wa Hully City (kulia)
aliomba msamaha kwa kujiangusha ili kupata penalti walipocheza dhidi ya
Crystal Palace Desemba 10, 2016
FA imesema kuwa jopo la wataalam litakaa kujadili namna ya kushughulikia suala hilo, huku tukio zima likirudiwa kutizamwa na mwamuzi, meneja wa timu pamoja na mchezaji mwenyewe kabla ya kutolewa kwa hukumu.
Kama kila mmoja ataridhishwa juu ya mbinu za uongo zilizotumiwa, mchezaji husika atafungiwa michezo miwili.
SHARE









No comments:
Post a Comment