Bwawa la Maji la Kunyweshea mifugo likiwa kwenye eneo ambalo ni karibu na sehemu ya Kiwanda cha kuchenjulia Dhahabu.
………………………………………………………
Wananchi
wa Kijiji cha Hililika Kata ya Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita
wameandamana kupinga mwekezaji kuweka kiwanda cha kuchenjulia Dhahabu
kwa madai kuwa chanzo cha maji ambacho wanakitegemea kijijini hapo kipo
karibu na planti ambayo inajengwa na kwamba inaweza kusababisha
madhara ya afya kutokana na Kemikali yaCyanide ambayo hutumika kwenye shughuli za uchenjuaji.
Wakizungumza na mtandao wa maduka online kwa vipindi Tofauti wamesema kuwa hofu kubwa waliyonayo
ni kutokana na sumu ya kuchenjulia dhahabu kwani ni hatari kwa afya zao
na viumbe ambavyo vinazunguka maeneo ambayo wanafanyia kazi.
“Sehemu hii ni karibu sana na eneo ambalo tunachotea maji sasa kama wakiweka hicho kiwanda
sisi wananchi tutakuwa kwenye hali gani hebu serikali ijaribu kulitazama
swala hili kwa umakini zaidi tutaisha kutokana na sumu ya kuozesha
marudio”Alisema Bi,Hellen Mbaru.
“Sawa
eneo hili ni la mtu Binafisi na lipo ndani ya kijiji cha Hililika na
kwamba tunaambiwa kuwa watawapa angalizo wawekezaji ndani ya mwaka mmoja
endapo kama kuna maafa ambayo yatajitokeza watawafukuza kweli na hali
hii jamani hadi watu wadhurike ndio tahadhili ichukuliwe mimi naomba
sana serikali ilitazame hili”Alisema
Hata hivyo lawama nyingi zimemwangukia Mwenyekiti wa Kijiji kuwa amehusika kwa kiasi
kikubwa Kwa kuchukua rushwa kutoka kwa mwekezaji na kwamba kwa sasa hawana
imani naye hali ambayo imesababisha kufunga ofisi ya Kijiji.
Kutokana na hali hii askari Polisi wamefika kwenye eneo hilo na kumshauri Mwenyekiti wa
Kijiji hicho ambaye alifika kwenye eneo hilo kuona umuhimu wa kuwasikiliza wananchi na kusitisha ujenzi wa Planti hiyo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Daniel Mwigulu Nkela,amesema kuwa maamuzi ambayo
yalichukuliwa hayakuwa ya peke yake bali ni ya wajumbe wote ambao waliridhian eneo hilo.
“Maana ya serikali kuna wajumbe 25 mimi kama mwenyekiti sina mamlaka ya kuidhinisha eneo
hili peke yangu mwekezaji anapotaka kuingia tunaitisha serikali ya
kijiji inakaa na inapokaa kuna kuwa na mahojiano kati ya mwekezaji na
wajumbe wa serikali ya kijiji mimi kazi yangu ni kulinda maadhimio
kikao tu sina mamlaka ya kuhidhinisha eneo lolote lile”Alisema
Mwigulu.
Maduka
online imemtafuta mwekezaji wa eneo hilo kutaka kujua makubaliano yake
na serikali ya kijiji ambapo moja kati ya wasimamizi wa eneo wamegoma
kuzungumzia swala hilo na kwamba
anaye weza kuzungumzia swala hilo ni meneja wao ambaye yupo Mwanza kwa
sasa hata hivyo jitihada bado zinaendelea kujua makubaliano yalikuwaje.
|
No comments:
Post a Comment