Waziri
wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Ubalozi wa
Tanzania Nairobi Kenya na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania
Nchini Kenya Mheshimiwa Balozi Mteule Dkt. Pindi Hazara Chana.
Prof.
Kabudi alifanya ziara hiyo tarehe 4/5/2017 wakati akihudhuria Mkutano
wa 56 wa Mwaka wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi
za Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organisation –AALCO)
unaofanyika mjini Nairobi.
Katika
ziara hiyo Prof. Kabudi aliongozana na Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda
Balozi Mteule wa Tanzania Nchini India yalipo makao makuu ya Jumuiya
hiyo na maafisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Prof.
Kabudi alimpongeza Balozi Pindi Chana kwa uteuzi na alishukuru kwa
maandalizi waliyoyafanya kuhakikisha ujumbe wa Tanzania unashiriki
ipasavyo mkutano huo. Vile vile alimuhakikishia kuwa Wizara ya Katiba na
Sheria pamoja na taasisi zake zitampa ushirikiano stahiki katika
utekelezaji wa majukumu yake, na kwamba Ubalozi uwe tayari kwa kufuata
taratibu zilizopo kiserikali kuwasiliana na Wizara pindi yanapoibuka
masuala yanayohitaji ushiriki wa Wizara.
Kwa
upande wake Balozi Dkt. Pindi Chana alimshukuru Prof. Kabudi kwa
kutenga muda kuja kuutembelea Ubalozi na kumpongeza kwa uteuzi
alioupata. Balozi Chana alimuahidi Prof. Kabudi kuwa Ubalozi utaendelea
kushirikiana ipasavyo na Wizara kwa kutumia taratibu zilizopo
utahakikisha kuwa masuala ya Wizara yanaifikia Wizara kwa wakati.
SHARE
No comments:
Post a Comment