TRA

TRA

Friday, May 19, 2017

Halotel yatoa ufafanuzi kesi ya makosa uhujumu uchumi.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Taarifa kwa vyombo vya habari
 

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu kuhusika na baadhi ya makosa yaliyohusishwa na kampuni hiyo pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, huku wakifafanua kuwa wao kama kampuni wamehusishwa na vipengele viwili vya mashitaka ambavyo ni, kushindwa kutoa taarifa za usajili wa kampuni ya UNEX Company Ltd, kwa ajili ya kusajili laini za simu 1000 zilizouzwa kwa kampuni hiyo. 

Pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri kwa kuuza laini za simu 1000 kwa kampuni ya UNEX ambayo haikuwa kampuni iliyosajiliwa kikamilifu ambayo bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walisimika mitambo ambayo iliwezesha kutumia laini hizo za simu kufanya mawasiliano nje ya nchi na kusababisha hasara ya sh. milioni 459 kwa serikali.

Kampuni hiyo pia, Imefafanua kuhusika na makosa mengine ambayo yamehusishwa na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na usimikwaji wa mitambo ya mawasiliano pamoja na makosa mengine ambayo yaliwahusisha watuhumiwa wengine ambao walikuwa ni wateja wa kampuni hiyo. 

Kampuni hiyo imesemainafanya shughuli zxake kwa kufuata taratibu na sharia za nchi na haijawahi kuwa na mitambo yoyote inayofanya mawasiliano kinyume na taratibu za mamlaka ya TCRA.


Katika Hati ya Mashtaka iliyosainiwa na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali tarehe 16 Mei, 2017, imeitaja kampuni ya Viettel (Halotel) kuhusika na makossa hayo katika kifungu namba sita (6) na namba saba (7) ambavyo havijauhusisha kampuni hiyo na makosa ya washtakiwa wengine ambao si wafanyakazi wa kampuni hiyo na wala hawana ushirikiano wowote na kampuni hiyo na raia hao wa Pakistani, Zaidi ya kuwauzia laini za simu kampuni hiyo kwa kuwakilisha nyaraka zisizo halali.


"Sisi ni kampuni inayofanya kazi kwa usajili na vibali halali tulivyopewa na mamlaka ya nchi hii na tumekuwa wawazi na kufuata taratibu na sheria, Mitambo iliyotumika katika kuiba mawasiliano ya simu haikuwa mitambo yetu na hatukufahamu kama wateja wetu (UNEX) walitumia mitambo hiyo kuiba mawasiliano, Hatuna uhusiano wowote na washitakiwa wengine ambao tumehusishwa nao, na wala sio wafanyakazi wa Halotel kama ambavyo imenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari n ahata mitambo hiyo sio ya kwetu” Alisema Mkurugenzi huyo.


Kampuni hiyo imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha na kuhakikisha huduma bora za mawasiliano kwa Watanzania, kwa kuendelea kupanua huduma zake kwani hadi sasa wameweza kufikia zaidi ya asilimia 95 ya watanzania wote na wanaendelea kutoa huduma bora zenye gharama nafuu.

Le Van Dai amesema kuwa kampuni hiyo imefanya uwekezaji mkubwa sana ndani ya nchi hivyo haiwezi kujihusisha na vitendo vingine vyovyote vinavyoweza kusababishia nchi hasara au kukiuka taratibu na sheria zilizowekwa na mamlaka husika.




Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Mawasiliano ya  Halotel, Tawi la Dar es Salaam, Daimon Malaki, akiwaeleza wafanyakazi wenzake kutoka idara mbalimbali za kampuni hiyo namna minara ya mawasiliano ya simu za mkononi inavyofanya kazi

Tumeweza kuunganisha mtandao wa intaneti kwa shule 417, Halmashauri za wilaya 123, hospitali 81, vituo vya polisi 131 pamoja na ofisi za posta 68.

Uwepo wetu ni maendeleo ya matunda ya ushirikiano mzuri baina serikali ya nchi mbili ya Tanzania na Vietnam, hivyo tunaamini kuwa ushirikiano huu utaendelea kuzaa matunda zaidi, na watanzania wengi kuendelea kunufaika kupata huduma bora za mawasiliano nchi nzima .

 

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger