TRA

TRA

Tuesday, May 9, 2017

Kabila apuuza upinzani na kutangaza baraza jipya la mawaziri

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila ametangaza baraza la mawaziri la mpito, akikaidi matakwa ya wapinzani wanaomtuhumu kwa kukiuka makubaliano ya awali. 

Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001, mwishoni mwa mwaka jana alifikia makubaliano na upinzani kuhusu kuendelea kwake kubaki madarakani baada ya muhula wake wa mwisho kumalizika, lakini makubaliano yao yalivunjika mwezi Machi mwaka huu. 



                Rais Joseph Kabila

Orodha ya watu 60 waliotangazwa katika nafasi za mawaziri na manaibu waziri inajumuisha majina mengi yaliyokuwa katika mabaraza yaliyotangulia, na wizara muhimu kama ya mambo ya nje, mambo ya ndani, sheria na migodi zimekwenda kwa wapambe wa Rais Kabila. 

Baraza jipya litakabiliwa na changamoto kubwa, zikiwemo kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Faranga, na uhaba wa raslimali inayohitajika kuandaa uchaguzi mkuu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

 CHANZO: DW

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger