Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisamiliana na
Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha alipowasili katika viwanja vya
Mahakama Kuu-Arusha kukamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Kaimu
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mhe. Kamugisha
akimsomea taarifa ya hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo.
Lengo la ziara ya Mhe. Kaimu Jaji Mkuu katika Kanda hiyo ni kujifunza na
kuona hali halisi ya mazingira ya kazi na utekelezaji wa majukumu.
Naibu
Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Rumisha (wa kwanza kulia)
akimuonesha Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, moja ya kumbi za Mahakama Kuu, Kanda
ya Arusha pindi alipokuwa akikagua ofisi mbalimbali za Mahakama ya Mkoa
na Mahakama Kuu katika Kanda hiyo.
Kaimu
Jaji Mkuu, Prof. Juma akiwa katika Kompyuta Mpakato akikagua Mfumo wa
Kuratibu takwimu za Mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS)
kuhakikisha kama inafanya kazi ipasavyo, pembeni ni Afisa TEHAMA,
Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Bw. Athuman
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania, akiongea na Mahakimu na Watumishi wengine wa
Mahakama (hawapo pichani), katika maongezi yake na Watumishi hao Mhe.
Jaji Prof. Juma amewataka na kuwasisitiza Watumishi hao kufanya kazi kwa
kuzingatia Maadili ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa
Wateja/Wananchi wanaowahudumia. kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu-Kanda ya Arusha na kushoto ni Mhe. Rumisha, Naibu Msajili-Mahakama
Kuu, Kanda ya Arusha.
Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza nao.
Mtendaji,
Mahakama Kuu-Arusha, Bw. Edward Mbara akiwasilisha taarifa ya hali ya
utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo mbele Mhe. Kaimu Jaji Mkuu na
Watumishi wa Mahakama, katika taarifa yake Bw. Mbara alikiri kuwa Kanda
ya Arusha inakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu chakavu ya
majengo ya Mahakama n.k (picha na Mary Gwera,Arusha)
SHARE
No comments:
Post a Comment