Korea Kaskazini
imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira yataruhusu
,kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini.
Mjumbe
mwandamizi wa Korea Kaskazini amesema kuwa mazungumzo na serikali ya
rais Trump yanawezekana kufuatia mkutano na waliokuwa maafisa wa
serikali ya Marekani nchini Norway.Awali mwezi huu rais wa Marekani Donald Trump alisema itakuwa heshima kubwa kukutana na rais Kim Jong un.
- Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
- Trump asema Korea Kaskazini ni tatizo
- Trump aionya tena Korea Kaskazini
Choe Son Hui ambaye ni afisa katika wizara ya maswala ya kigeni kuhusu maswala ya Marekani kaskazini alitoa matamshi hayo wakati alipokuwa akirudi Pyongyang baada ya mkutano mjini Oslo.
SHARE
No comments:
Post a Comment