TRA

TRA

Monday, May 29, 2017

MASHINDANO YA EUROPEAN YOUTH FILM COMPETITION (EYFC) 2017 YAZINDULIWA RASMI.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Mashindano yanayoitwa European Youth Film Competition yamezinduliwa rasmi leo, May 29, 2017 ambapo yatafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza.

Mashindano hayo yameandaliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na washirika nchi za Netherlands, United Kingdom, Ubalozi wa Ufaransa, Alliance Française, British Councils pamoja na Bodi ya Filamu nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya (EU), Susanne Mbise amesema katika shindano hilo vijana watapata fursa ya kuzungumzia mijadala ya maendeleo wakati watakapokuwa wakizungumzia Suala la Ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania, Afrika na Duniani. Swali likiwa Je suala hilo ni changamoto au fursa ya maendeleo?

"Ndani ya Filamu za dakika 5 au 10 Washiriki wanatakiwa kuandaa Filamu ya aina yoyote, iwe 'Documentary', Maigizo lakini iwe dakika 5 au 10 katika Maudhui hayo", amesema Mbise.

Mbise amesema kuwa Kati ya vijana hao wenye umri kati ya miaka 18-35 watashindana na Washindi wa tano bora watakwenda kwenye Mashindano makubwa.

Kwa upande wa Bodi ya Filamu nchini, Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Abuu Kimario amewapongeza Umoja wa Ulaya kwa kuandaa Mashindano hayo, kwani yamekuja siku muafaka, kutokana na Soko la Filamu linapanda na kushuka.

Naye Mratibu wa Mashindano hayo, Moses Saka amesema kuwa mshindi wa kwanza katika Shindano hilo atazawadiwa kiasi cha Shilingi Milioni 7, mshindi wa pili Sh. Milioni 5, na mshindi wa tatu Sh. Milioni 3 za Kitanzania.
 Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya (EU), Sussane Mbise (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya European Youth Film Competition (EYFM) yanayozinduliwa May 29. Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi ya Filamu nchini, Abuu Kimario, Kushoto ni Mratibu wa Shindano hilo, Moses Saka.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger