Baada ya Miss Tanzania 2o16 Diana Edward kukabidhiwa
zawadi ya gari aliloahidiwa kufuatia ushindi kwenye shindano
lililofanyika October 2016, gari hilo limekuwa gumzo mitandaoni kutokana
na mabango yaliyowekwa kwenye gari hilo.
Kupitia Leo Tena ya Clouds FM leo May 12, 2017 Miss Tanzania 2016, Diana Edward amesema
anatoa shukrani na anawaunga mkono waandaaji na hawezi kuwazuia watu
kusema kwa kuwa hawafahamu namna gani wamepambana kulipata gari hilo.
“Mabango
yatatolewa siku hizi mbili na nimefundishwa kushukuru. Kwa hiyo,
nilichopewa nimeshukuru. Nitaliendesha gari, sina kipingamizi. Maneno,
watu watayaongea, hiyo ipo. Hakuna binadamu anayekubali kitu. Ndio uwezo
wao ulipofikia wa kunipa hiyo zawadi.
“Siwezi
kuwapinga – ninawaunga mkono. Mimi ni binadamu pia, kwa hiyo, nimepewa
zawadi na nimepokea kwa shukrani, na nawashukuru Kamati na wadhamini na
watu wote walioshiriki mpaka nikapata gari.
“Sijui
wanachokiongea, ila hali halisi ndio hiyo. Niliitwa nikaambiwa gari
lako ndio hili. Nikalipokea kwa shukrani. Mimi sijali watu wanasema
nini, maana maneno yapo. Wao wamenipa walichokiweza kwa sababu
wamehangaika kweli kulitafuta hilo gari. Watu hawawezi kujua kwa sababu
wapo kwenye social media, lakini wangekuwepo tangu watu wanahangaika
kulipata hilo gari tangu mwezi wa 6 mpaka leo hii wmaepata.” – Diana Edward.
SHARE
No comments:
Post a Comment