NA MADUKA ONLINE
MKUU wa
Mkoa wa Geita Meja Jenereli Mstaafu Ezekiel
Kyunga amezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitano ambapo mitatu ni vituo vya afya na viwili ni shule moja na Mabweni kwenye shule ya sekondari
Kasamwa.
Kyunga amezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitano ambapo mitatu ni vituo vya afya na viwili ni shule moja na Mabweni kwenye shule ya sekondari
Kasamwa.
Akielezea
Miradi hiyo yote Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mhandisi Modest
Aporinali amesema bajeti ambayo waliyonayo kwa kila kituo cha afya
wametenga kiasi cha sh ,Milioni Miamoja na kwamba mahitaji ni
vituo vya afya kumi na kwasasa ni vituo viwili ambavyo vinafanya kazi.
vituo vya afya kumi na kwasasa ni vituo viwili ambavyo vinafanya kazi.
“Ni kweli
Halamshauri yetu inauwitaji Mkubwa sana wa Vituo vya afya ingawa kwa sasa tunavyo
vituo viwili ambavyo ni Nyankumbu na Kasamwa ambavyo vinafanya kazi hata hivyo
mmeona tumezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye vituo vitatu ambapo ni
Mpomvu,Nyanguku na Shiloleli tutaendelea na jitihada kwa kutumia mapato yetu ya
ndani ili kupunguza changamoto ya vituo vya afya hata hivyo GGM
wametupa msaada kama milioni mia moja kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mgusu”Alisema Modest.
wametupa msaada kama milioni mia moja kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mgusu”Alisema Modest.
Hata
Hivyo Mkurugenzi Modest ametaja miradi ya shule ambazo zimewekewa mawe ya
msingi kuwa ni shule ya Msingi Tumaini pamoja na Mabweni kwenye shule ya
sekondari Kasamwa na kwamba wanaendelea na juhudi ya kupambana na changamoto za
elimu kwenye
Halmashauri ya Mji.
Halmashauri ya Mji.
Mkuu wa
Mkoa ,Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga ,amesisitiza kuwa serikali inafanya juhudi
za kuwashirikisha wananchi katika swala la maendeleo na kwamba wanatakiwa kuwa
na mwitikio katika swala la maendeleo kwa wao kama wananchi kwa kujitolea
bila ya kusubilia serikali huku
akiwataka baadhi ya watu kutokuwa na desturi ya kulalamika bila ya kufanya shughuli kwa kushirikiana na Serikali.
akiwataka baadhi ya watu kutokuwa na desturi ya kulalamika bila ya kufanya shughuli kwa kushirikiana na Serikali.
Aidha kwa
upande wao wananchi ambao wamezungumza na maduka online Habari wameipongeza serikali
kwa hatua nzuri ya kuwapelekea vituo vya afya kwenye maeneo yao huku
wakielezea changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili kabla ya kuwepo kwa vituo vya afya kuwa ni umbali mrefu wa kufuata huduma ya afya.
wakielezea changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili kabla ya kuwepo kwa vituo vya afya kuwa ni umbali mrefu wa kufuata huduma ya afya.
Jumla ya miradi
yote ambayo imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi imeghalimu kiasi cha Sh,Milioni
Mia saba na thelasini na sita pesa ambazo zinatokana na mapato ya
ndani.
ndani.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiweka Jiwe la Msingi kwenye shule Mpya ya Msingi ya Tumaini Iliyopo kwenye Mtaa wa Nyantorontoro A Kata ya Nyankumbu Wilayani Geita. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza wananchi kuwa ni watu wa kujitolea kwenye maendeleo na kuachana na itikadi za kisiasa ambazo zimekuwa zikirudisha jitihada za maendeleo Nyuma. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita akikagua chumba cha Darasa kwenye shule ya Msingi ya Tumaini |
Mkuu wa Mkoa akiwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mkurugenzi pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji kwa juhudi ambazo wamezifanya . |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha afya cha Mpomvu kilichopo kwenye Kata ya Mtakuja. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo cha afya. |
Kituo cha afya cha Nyanguku |
Bwalo la chakula kwenye shule ya Sekondari ya Kasamwa ambayo pia Mkuu wa Mkoa aliweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Bwalo pamoja na Mabweni. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiweka Jiwe la Msingi Kwenye Mabweni na Bwalo shule ya sekondari ya Kasamwa. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Akikagua baaadhi ya Mabweni kwenye shule ya Sekondari ya Kasamwa. |
Baadhi ya Mabweni ambayo yanaendelea Kujengwa kwenye Sekondari ya Kasamwa . |
SHARE
No comments:
Post a Comment