NA MATUKIODAIMABLOG
UTEKELEZAJI kwa
vitendo wa agizo la makamu
wa Rais Samia Suhulu Hassan la
kufanya mazoezi kila jumamosi
moja ya mwezi kwa ajili ya
kuepukana na magonjwa yasiyo ambukiza ,umemvutia mstahiki
meya wa kinondoni Beny Sitta mkoani Iringa.
“ Nimekuja
kwenye semina kwa
kuwa mkuu wa wilaya ya
Irina Richard Kasesela
ni kaka yangu nilimuomba kuwa
nahitaji kushiriki mazoezi ili kuona utaratibu wenu wa mazoezi mkoa wa Iringa
basi akaniambia amka asubuhi ili
uone sisi tulivyofika mbali kweli nimeshuhudia na nimejifunza
kitu ila wakati nafanya
mazoezi kila nikimtazama mkuu wa mkoa naona
bado anaendelea na mazoezi name nikawa naona aibu ndio maana nimevumilia hadi mwisho kweli nawapongeza sana kwa kweli mmefika mbali “
Mkuu wa wilaya ya
Iringa Richard Kasesela alisema kuwa wananchi
wa mji wa Irina hasa Manispaa
ya Irina wamekuwa wakijitoa zaidi katika
ushiriki wao kwenye mazoezi hayo
na kuwa kila jumamosi saa 12;00
asubuhi wananchi wamekuwa wakijitokeza
ofisi ya mkuu wa mkoa kwa akuanza mazoezi ya kukimbia hadi uwanja wa Samora
umbali wa kilomita 3 kutoka ofisi ya
mkoa hadi uwanjani ambako
huko hufanya mazoezi mbali mbali
ya viungo chini ya wataalam .
Huku mkuu wa mkoa
wa Irina Amina Masenza alisema kuwa wembe bado ni ule
ule katika mkoa wa Iringa hatapenda
kuona washiriki wa mazoezi wanapunguza zaidi atapenda kuona wananchi
wengi zaidi wanajitokeza katika uwanja
wa Samora kwa mazoezi .
Alisema mkoa wa Irina umekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila
jumamosi na jumamosi ya
mwisho wa mwezi ni jumamosi ya
Rais Dkt John Magufuli kwa maana ni
jumamosi ya usafi kitaifa na mkoa wa Iringa
umekuwa ukizingatia maagizo yote
ya viongozi wa kitaifa .
|
No comments:
Post a Comment