Rais Barrack Obama
alimuonya rais mpya wa Marekani Donald Trump dhidi ya kumteua Michael
Flynn kuwa mshauri wake wa maswala ya usalama wa kitaifa , ikulu ya
Whitehouse imethibitisha.
Bwana Obama alimuonya mrithi wake chini
ya saa 48 baada ya uchaguzi wa mwezi Novemba wakati wa mazungumzo katika
afisi ya rais, waliokuwa maafisa wa Obama wamesema.Mawasiliano ya bwana Flynn na mjumbe mmoja wa Urusi yalimfanya kuwa rahisi kufanya usaliti jopo la seneti liliarifiwa siku ya Jumatatu.
Alifutwa kazi mnamo mwezi Februari kwa kuficha mawasiliano hayo.
- Pizzagate: Msaidizi wa Trump apoteza kazi
- Mshauri wa Donald Trump ajiuzulu
- Michael Flynn kuchunguzwa?
Katibu wa maswala ya habari Sean Spiecer alisema kwamba ni kweli rais Obama aliweka wazi kwamba hakumpendelea Jenerali Flynn.
Lakini Spicer alisema kuwa hilo sio kujambo la kushangaza kwa kuwa jenerali Flynn alikuwa amefanya kazi na rais Obama na kwamba alikuwa mkosoaji mkubwa wa rais huyo hususan kwa kushindwa kwake kuwa na mipango ya kulikabili kundi la IS na vitisho vyengine vilivyokuwa vikikabili Marekani.
SHARE
No comments:
Post a Comment