Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF)Mhe. Anna Makinda akiwasili katika ukumbi wa Ledger Hotel
Jijini Dar es Salaam kufungua Kongamano la Kwanza la Bima ya Afya na
Kinga ya Jamii .
Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF)Mhe. Anna Makinda akizungumza wakati wa kongamano la
kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii lililofanyika jana Jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
wa Shirika lisilo la Kiserikali la Pharm Access Dkt. Heri Marwa
akizungumzia uhuhimu wa Sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika
kuboresha huduma za Afya hasa kwa wananchi wasio na uwezo.
Kamishna
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware akizungumza
wakati wa kongamano hilo kuhusu umuhimu wa kuwa na Sera ya Bima hapa
nchini ili kuwalinda wananchi .
Mkurugenzi
wa kuendeleza miradi, Pharm Access, Ewout Irrgng akizungumza wakati
wa akizungumza wakati wa kongamano la kwanza la Bima ya Afya na Kinga
ya Jamii lililofanyika Jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF)Mhe. Anna Makinda akifurahia jambo na Mkurugenzi msaidizi
anayeshughulikia Afya toka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Anna Nswilla
kabla ya ufunguzi wa kongamano la kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya
Jamii. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Kaimu
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii Slvery Mgonza akiwasilisha mada
katika kongamano la kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii,
lililofanyika Kunduchi katika hoteli ya Ledger plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali
ya Awamu ya Tano imepongezwa kwa kuimarisha na kuendeleza miundo mbinu
ya Afya,uboreshaji huduma kupitia teknolojia na Usambazaji wa madawa
hadi kwenye vituo vya kutolea huduma.
Kauli
hiyo ilitolewa jana Jijini Dar es Salaam na Spika mstaafu wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi Anna Makinda
wakati akifungua Kongomano la kwanza la bima ya afya na kinga ya jamii .
“’Lazima
tuangalie na kuwatambua wale ambao hawawezi kulipia huduma za afya na
tuangalie namna gani tutahakikisha wanapata huduma na isitokee wakati
wowote wengine wakpoteza maisha kwa kukosa fedha za kujiunga na Bima ya
Afya.’’ Alisisitiza Makinda.
Akifafanua
Makinda amesema kuwa kuna umuhimu wa kuangalia namna huduma
zinavyotolewa katika vituo vya kutolea huduma,upataikanaji wa vifaa tiba
na dawa,hali inayochochea upatikanaji wa huduma bora kwakuwa ndiyo
dhamira ya Serikali kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Kuhusu
Afya bora kwa wote Makinda alibainisha kuwa azma hiyo itafikiwa kupitia
utaratibu wa Bima ya Afya na na mpango wa CHF iliyoboreshwa katika
Halmashauri 50 hapa nchini.
Akizungumzia
mkakati wa kutoa huduma bora Makinda amesema kuwa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya umejipanga kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na watoa
huduma zinaendana na dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa kila mtanzania
anapata huduma bora za afya .
Aliongeza
kuwa watoa huduma watakao toa lugha zisizofaa kwa
wagonjwa,kuwanyanyapaa, kuonyesha tabia ya ukatili watafungiwa kutoa
huduma kama kituo hicho kimesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Kwa
Upande wake Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini Dkt.Baghayo
Saqware amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Sera ya Taifa ya Bima
itakayowezesha wananchi huduma bora za Afya.
“Sera ya Taifa ya Bima tasaidiakuondoa tatizo la watoa huduma za Bima wasio waaminifu “ alisisitiza Dkt.Saqware.Tanzania
kama nchi imekuwa na historia ndefu ya kutoa huduma bora za matibabu
kupitia bima ya Afya, Kuanzishwa kwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Bima Binafsi zikiwa ni juhudi za
kuboresha huduma hizo hapa nchini.
Kongamano
la Bima ya Afya na Kinga limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka
ya Udhibiti na Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) na shirika la Pharm
Access International.
SHARE
No comments:
Post a Comment