NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO, DAR ES SALAAM
WAKALA wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imeunda kikosi
kazi maalumu kitakachohusika na zoezi la ukusanyaji wa madeni ya kiasi cha Tsh
Bilioni 10 inazodai TEMESA katika taasisi za Serikali.
Hadi
kufikia mwezi machi mwaka huu TEMESA imekusanya kiasi cha Tsh milioni 157
inazodai kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali.
Hayo
yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu wakati wa mahojiano
ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari- MAELEZO
na kurushwa hewani na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC).
Dkt
Mgwatu alisema kuwa TEMESA ina jukumu la kutoa huduma za kiuhandisi kwa Taasisi
za Umma na watu binafsi ikiwemo uzalishaji na utengenezaji magari pamoja na
uboreshaji mitambo na huduma za vivuko na huduma za ushauri na uendeshaji.
“TEMESA
imekuwa ikiongeza vivuko kulingana na mahitaji ya huduma hivyo ina mpango wa
kuongeza kivuko kimoja katika eneo la Kigamboni na kufanya vivuko kuwa vitatu
vitakavyofanyakazi saa 24 kwa lengo la kurahisisha huduma ya usafishaji”
alifafanua Dkt. Mgwatu.
Aidha
alisema kuwa katika mwaka wa Fedha 2017/2018 TEMESA imepanga kuboresha zaidi
matumizi ya TEHAMA kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi ndani ya TEMESA na
kuboresha huduma ili kuwavutia taasisi na watu binafsi kupata huduma za taasisi
hiyo.
Vilevile
Dkt. Mgwatu aliongeza kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka 2017 TEMESA imepanga
kupunguza gharama za tozo za utengenezaji wa magari kwa taasisi za umma na watu
binafsi.
Mbali
na hayo Wakala wa Ufundi na Umeme nchini kwa mwaka 2016/2017 imeweza kutekeleza
miradi mbalimbali mikubwa iliyokamilika ndani ya muda uliopangwa ambapo
imeshiriki pia katika ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM).
SHARE
No comments:
Post a Comment