TRA

TRA

Wednesday, May 24, 2017

TIB YAANZA KAZI BANDARINI KWA MUDA WA SAA 24

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

Katika kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli benki ya biashara ya TIB imeanzisha huduma za kibenki kwa masaa 24 katika tawi dogo la benki hiyo lililopo katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege amesema huduma hiyo inawawezesha wananchi wote kulipia kodi za aina mbali mbali pamoja na tozo zote za bandari.

Amesema hivi karibuni TIB benki na TRA ziliingia mkataba kwa kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ambapo mtu akilipa kodi kupitia mfumo huo katika tawi lolote la benki hiyo, taarifa zake zitaonekana moja kwa moja kwenye mtandao wa TRA.

Amesema kuwa, benki hiyo ya biashara (TIB), ndiyo benki pekee yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya akaunti za TPA hivyo mwananchi atakapolipia tozo yoyote bandarini taarifa zake huonekana mara moja katika mtandao wake hivyo kurahisisha na kuwezesha kuendelea na taratibu zingine za utoaji mizigo kwa haraka zaidi.

“TIB bank inatoa huduma mbali mbali kutokana na mahitaji ya mteja, zikiwemo za akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya muda mfupi na muda wa kati dhamana za kibenki uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni na shughuli zote za kibenki”, amesema Nyabundege.

Aidha amesema, benki hiyo ya kibiashara yenye matawi 6 nchini, Dar esSalaam matatu, Mwanza, Arusha na Mbeya inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na pia inatoa huduma kwa watu binafsi taasisi binafsi na serikali.


Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya benki hiyo kufanya kazi saa 24 Bandari ya Dar es Salaam
Mkurugenzi mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya TIB  Theresia Soka akizungumzia ubora wa huduma hizo.
Watendaji wa Benki ya Biashara ya TIB
Sehemu ya Waandishi wa Habari walifika katika mkutano huo

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger