Mchezaji
wa timu ya Simba SC, Mohamed Hussein amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.Hussein
aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam
FC. Katika mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa
dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake
kubaki katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.Pia
alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.Kwa
kushinda tuzo hiyo, Kaseja atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000
(milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom
Tanzania.Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mwezi za Ligi Kuu ya
Vodacom msimu wa 2016/2017 ni John Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya
wa Simba (Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa
Ndanda (Novemba).Wengine ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma
Kaseja wa Kagera Sugar (Januari), Hassan Kabunda wa Mwadui (Februari),
Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu
Shooting (Aprili).
SHARE
No comments:
Post a Comment