Vijana kutoka mataifa mbalimbali
waliokusanyika katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la
Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN), mjini Arusha wametakiwa kuchambua
masuala yaliyopo mbele yao kwa makini ili kutoa jawabu kwa matatizo ya
dunia yanayohitaji ushiriki wao.
Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa serikali katika mkutano huo
Ngusekela Karen Nyerere, Ofisa anayeshughulikia dawati la Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Aliwataka vijana wanaoshiriki TIMUN kuhakikisha wanaangalia kwa makini
mambo yanayogusa nchi zao na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuwa ndio njia
pekee ya kutekeleza malengo endelevu ya dunia ambayo yanahitaji
ushirikiano wa ndani na wa kimataifa.
TIMUN ambayo kirefu chake ni Tanzania International Model United Nations
hufanyika kila mwaka na ujumbe mbalimbali na mwaka huu ujumbe wa TIMUN
ni: “kuwawezesha vijana katika diplomasia na uongozi” Picha
juu na chini ni Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza
Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaofanyika kwenye
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini
Arusha.[/caption]
TIMUN huandaliwa na Shirikisho la vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA)
taasisi ya vijana isiyotengeneza faida inayotangaza shughuli za Umoja wa
Mataifa na kushirikisha vijana katika utekelezaji wa shughuli hizo.
Aidha aliwashukuru waandazi wa mkutano huo kubwa unaofanana na Mkutano
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (General Assembly) wenye lengo la kukutanisha
vijana kujadili mustakabali wa malengo ya dunia.
Alisema vijana wana nafasi muhimu katika utekelezaji wa malengo hayo ya
maendeleo endelevu jukumu ambalo dunia imejipa kwa miaka 15 hadi mwaka
2030.
Pamoja na kuwashukuru Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson
Mandela, Arusha (NM-AIST) kwa kukubali kuwa mwenyeji wa kambi hiyo, hali
iliyoonesha kwamba wanajali vijana, mwakilishi huyo wa serikali alisema
kwamba Tanzania ipo tayari kusukuma mbele ajenda ya ushirikishaji
vijana katika maendeleo endelevu kwa kuwa inaamini juu ya hilo.
“Wakati serikali inafanyakazi kwa
karibu na taasisi nyingine kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo
yanatekelezeka, baraza la vijana ambalo litakutana litakuwa na kazi
kubwa ya kutengeneza sauti ya pamoja namna ya kukabiliana na changamoto
zilizopo”
Alisema kwamba malengo ya dunia ambayo yapo 17 yanagusa kila sehemu ya
maisha na hivyo ni vyema kama vijana watatoka na majibu ya maswali
yanaoumiza vichwa kuhusu malengo hayo hasa mazingira na dunia endelevu.
Aliwataka vijana kutumia nafasi yao vyema katika jukwaa hilo kwani
maisha ya watu bilioni 7 duniani wanategemea namna ambavyo wanajengwa na
vijana, wenye mchango muhimu wa kulinda mazingira na kuhakikisha
maendeleo endelevu. Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifungua rasmi Mkutano Mkuu
wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa
(TIMUN-2017), unaofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya
Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha[/caption]
Awali Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba
zaidi ya vijana elfu 20 nchini Tanzania wamefunzwa malengo endelevu ya
dunia, toka ulipofanyika uzinduzi Juni, 2016.
Akizungumza katika hafla ya kambi ya mwaka huu ya Tanzania International
Model United Nations (TIMUN), inayofanyika katika Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST), Bw. Rodriguez alielezea
kufurahishwa na idadi hiyo ya vijana waliohamasishwa na kusema kwamba
malengo ya maendeleo endelevu 2030 yanahitaji kila mmoja kushiriki.
Aidha alielezea umuhimu wa ushiriki wa vijana katika masuala ya
maendeleo kutokana na uwingi wao hapa nchini. Asilimia 67 ya watu nchini
ni vijana. Mkutano
ukiendelea katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson
Mandela (NM-AIST) jijini Arusha.[/caption]
Bw. Rodriguez alishukuru machampioni kwa kuwezesha vijana wenzao
kutambua malengo endelevu ya dunia na kuwataka kuendelea kufanya vizuri
zaidi katika kuwashawishi vijana wenzao kuelewa na kushiriki katika
malengo hayo.
“Nataka kuwatafadhalisha kwamba huu ni mwanzo tu, kuna mengi ya
kufanya. Kama Umoja wa Mataifa, tunawataka wote mshiriki, si tu katika
kuelimisha kuhusu malengo haya ya dunia, lakini pia katika kuangalia
mwenendo wa maendeleo hayo katika jamii na namna yanavyotekelezwa. Tukio
kama hili la TIMUN linasaidia kuongeza uwezo wa kufikia malengo ya
dunia,” alisema Bw. Rodriguez.
Vijana 50 wa kwanza machampioni walifunzwa mwaka jana katika TIMUN 2016.
Kwa sasa kuna vijana machampioni 500 nchini Tanzania ambao wamepeleka
ujumbe kwa vijana wenzao 20,000. Mratibu
wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa
Mataifa (TIMUN 2017), Tajiel Urioh akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo unaoendelea jijini Arusha.[/caption]
Ujumbe ambao umekuwa ukisambazwa na machampioni kwa wenzao umeelezwa
kulenga kuchochea hamasa ya kuelewa malengo kwa ajili ya maendeleo.
“Kama watu hawatajua malengo ya maendeleo endelevu, hawataweza kufanya malengo hayo kuwa ya kweli,”
aliusema ujumbe huo Gloria Nassary, ambaye ni mmoja kati ya vijana 50
waliopewa mafunzo ya kwanza ya kuwa machampioni wa malengo ya dunia.
Naye Tajiel Urioh ambaye ni Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa
Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017), pamoja na
kusisitiza amani kama sehemu muhimu ya kusukuma mbele utekelezaji wa
malengo 17 ya maendeleo endelevu aliwahimiza vijana kutokata tamaa
katika kuhimiza utekelezaji wa malengo hayo. Ofisa
wa Mawasiliano NUNV anayeshughulikia tovuti na mitandao ya kijamii
katika ofisi ya Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini, Edgar Kiliba akiendesha kipindi cha maswali na majibu wakati wa
Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa
(TIMUN 2017) unaoendelea jijini Arusha kwenye ukumbi wa Taasisi ya
Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini
Arusha.[/caption]
Alisema bila amani kuanzia katika ngazi ya familia, uwezekano wa
kutekeleza malengo hayo unakuwa mgumu kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati
ya amani na utekelezaji wake.
Alisema amani ni kionjo muhimu cha maendeleo kinapokosekana hata jukumu
la vijana kulinda mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu
halitawezekana.
Alisisitiza kulinda mazingira kwa ajili ya maendeleo na kufikiwa kwa
malengo ya Umoja ya Mataifa ambayo ni malengo ya dunia katika kuimarisha
ustawi wa jamii na kuinua uchumi .
Urioh katika mazungumzo yake alisema suala la uchafuzi wa mazingira ni
suala gumu na mtambuka na kwamba mabadiliko ya tabia nchi
yanayosababishwa na kuvurugwa kwa tabaka la ozoni halihusu Ulaya pekee,
ambao wanachafua bali kila mmoja duniani; akiongeza kuwa mwishoni mwa
siku wanaoathirika ni zaidi nchi zinazondelea akitolea mfano nchi za
kusini mwa Jangwa la Sahara. Championi
wa Malengo ya dunia (Global Goals) nchini, Rio Paul akitoa maoni katika
Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa
Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea jijini Arusha.[/caption]
Alisema suala la kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi si kutulia bali
kuwajibika kutekeleza wajibu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba
hakuna uharibifu wa mazingira unaofanyika katika taifa la Tanzania.
Alisema vijana wanaweza kufanya zaidi ya yale ambayo kwa sasa
wameyafanya katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu kwa
kuhakikisha kwamba wana elimu ya kutosha kuhusu malengo hayo na
kushirikiana kuyatekeleza kwa kuangalia changamoto mbalimbali ambazo
wanazipatia majibu.
Alisema lengo la malengo hayo ni kusaidia jamii vivyo hivyo vijana nao
wanatakiwa kujitoa mhanga kuhakikisha kwamba jamii inaendelea kustawi na
kuendelea kwa manufaa ya kizazi kijacho.
[caption id="attachment_2117" align="aligncenter" width="1404"] Mmoja
wa washiriki kutoka nchini Uingereza akiuliza swali kwa Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo.[/caption]
Aliwataka vijana kutafuta majawabu ya mambo yanayoikabili dunia kwa
namna ya busara na kitaalamu zaidi huku wakizingatia diplomasia.
Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya
malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu.
Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15
ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa
namna ya kuwa endelevu. Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiteta jambo na Mwenyekiti wa
Shirikisho la vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini, Jacqueline
Kamwamu wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli
la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea mjini Arusha.
Kushoto ni Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la
Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017), Tajiel Urioh[/caption]
Wakati akiwa Arusha, Mratibu pia alifuatilia matokeo ya mafunzo
yaliyofanyika Novemba mwaka jana katika chuo kikuu cha Tumaini Makumira
yaliyofanywa kwa pamoja kati ya Umoja wa mataifa na Jumuiya ya Ulaya.
Katika mafunzo hayo machampioni 80 walifunzwa wakiwemo wanachuo 30
kutoka Taasisi ya Uhasibu ya Arusha (Institute of Accountancy Arusha
-IAA).
Mkutano huo umefadhiliwa Umoja wa Mataifa (UN), Serikali, Covenant Bank,
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia
ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) pamoja PIU. Katibu
wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wa Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akijibu baadhi ya maswali
kutoka kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Pichani
juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi
wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la
Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea mjini Arusha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisalimiana na Kaimu
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela,
Arusha (NM-AIST) anayeshughulikia Fedha, Mipango na Utawala, Dr. Musa
Chacha (kushoto) baada ya kuwasili ofisini kwa Makamu Mkuu wa Taasisi
hiyo, Prof. Karoli Njau (katikati) jijini Arusha. Makamu
Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha
(NM-AIST) Prof. Karoli Njau akiwa kwenye mazungumzo ofisini kwake na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia)
aliyeambatana na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce
Temu (wa kwanza kulia), Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen
Nyerere, Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa pamoja na
Ofisa wa Mawasiliano NUNV anayeshughulikia tovuti na mitandao ya kijamii
katika ofisi ya Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini, Edgar Kiliba. Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi Makamu Mkuu wa
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST)
Prof. Karoli Njau kitabu chenye taarifa na ripoti mbalimbali za Umoja wa
Mataifa baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la
Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea mjini humo. Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa na mwenyeji wake Makamu
Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha
(NM-AIST) Prof. Karoli Njau wakieleka kwenye eneo maalum la kupiga picha
kwenye taasisi hiyo. Meza
kuu kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la
Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) katika picha ya pamoja. Meza kuu katika picha ya pamoja na waandaaji wa TIMUN 2017. Picha ya pamoja na washiriki wa TIMUN 2017 kutoka nje ya Tanzania. Picha ya pamoja na washiriki wa kambi ya TIMUN 2017 inaoendelea jijini Arusha.
MISS TANZANIA SUPER MODEL AWASILI CHINA
Mshindi wetu wa Miss Tanzania Super Model 2017, Asha Mabula tayari
amewasili Macau, China akiiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya
"World Super Model". Tufungue Facebook page ya "World Super Production"
na "ku-like" picha zake kwa wingi ili kumwongezea points za ushindi.
Viva Asha
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
SHARE
No comments:
Post a Comment