Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo Tanzania (TAJF), Gerald
Kitabu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa TAJF
wakati wa kikao kilichofanyika Ufukwe wa Malaika Beach Resort jijini
Mwanza jana kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.
Katibu wa Chama hicho, Elias Msuya akizungumza katika kikao hicho. Kulia ni Mtunza Fedha wa chama hicho, Ellen Manyangu.
Wanachama wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Mwanza
WAANDISHI
wa Habari wanaounda Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo wamekutana
Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili mambo
mbalimbali ya chama hicho.
Akizungumza
katika kikao hicho kilichofanyika jana Mwenyekiti wa chama hicho,
Gerald Kitabu pamoja na mambo mengine alihimiza wanachama ambao bado
hawajatoa michango yao ya mwaka waitoe ili kutunisha mfuko wa chama
hicho.
“Ni muhimu wanachama ambao bado hawajaotoa michango yao kuhakikisha wanaitoa kwa wakati” alisema Kitabu.
Katibu wa
Chama hicho, Elias Msuya alisema chama hicho kipo katika mchakato wa
kutengeneza vitambulisho kwa ajili ya wanachama na wakati wowote
vitakapo kuwa tayari vitatolewa kwa wahusika.
SHARE
No comments:
Post a Comment