Mjadala wa jana jioni wa wagombea katika kinyang'anyiro
cha urais huko nchini Ufaransa ambapo raia wa nchi hiyo wanatarajiwa
kumchagua rais mpya mnamo siku ya Jumapili ulijawa na kejeli, matusi na
kushambuliana
Jioni hiyo mjadala kati ya Macron na Le Pen ulikuwa mkali. Wagombea
hao wa urais waliweka historia katika siasa za Ufaransa. Haijawahi
kutokea kwa wagombea wawili kutupiana maneno makali na ya uadui. Hasa ikizingatiwa kuwa Emmanuel Macron ndio mgombea mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushiriki katika kinyanyang'anyiro cha urais nchini Ufaransa na huku Marine Le Pen akiwa ndie mwanasiasa aliyetumia kauli za uogno kwa muda wa saa mbili na nusu mbele ya kamera za waandishi wa habari.
Macron mgombea urais mwenye siasa za mrengo wa shoto alionyesha kuwa na nguvu.
Alikuwa amejitayarisha vizuri kuliko ilivyotarajiwa kwa sababu kumkabili mpinzani mwenye uzoefu kwenye medani za kisiasa ni kama kupambana na kifaru vitani kwa mikono mitupu. Lakini Macron pamoja na tabia yake ya upole alionyesha kuwa ni sawa na chuma.
Alimmaliza Le Pen kama vile Le Pen alivyojaribu kummaliza yeye, Macron alimshambulia kwa kumwita kupe anayefyonza mfumo wa kisiasa, na mrithi wa nasaba za itikadi kali za mrengo wa kulia,alimwita pia ni muhubiri wa chuki na mtu anayependa kuwatia watu wasiwasi.
Kwa upande wake Marine Le Pen ni wazi kutoka mwanzo alimmwagia matusi mpinzani wake na alimshutumu kuwa yeye ni mwanafunzi wa rais Hollande alimtaja kuwa ni mtu mwenye kuchukia watu na mtumwa wa soko la fedha. Pengine Le Pen alidhani Macron atashikwa na hasira au angeweza kupoteza ujasiri wake lakini haikuwa hivyo Macron hakuyumba na aliendelea kushiriki vizuri kama yeye.
Nguvu za mgombea huyo huru ziko katika sera za kiuchumi. Aliweza kuuonyesha udhaifu wa misemo ya Le Pen alisema hajui jinsi makampuni yanavyofanya kazi, hajui nini hasa maana ya fedha, haelewi jinsi uchumi wa Ufaransa unavyoendelea wala hajui jinsi ya kupambana na ukosefu wa ajira. Macron alimsukuma mkuu huyo wa chama cha National Front hadi ukutani.
Karibu asilimia 40 ya wapiga kura wa Ufaransa ambao wanapanga kumchagua Le Pen wasiwe wapumbavu kwa kuamini ahadi za chama cha National Front.
Wanataka kuwa ndio wenye nguvu duniani kwa kuahidi kufanya kazi kidogo, kustaafu mapema, kusiwepo na ushindani. Baadhi ya watu nchini Ufaransa wana ndoto ya kuwa peponi jinsi wanavyoota wale wanaopendelea siasa kali za mrengo wa kulia.
Thamani na burudani ya mjadala huo ilikuwa kubwa. Lakini je watazamaji walijifunza kitu gani? Mwishowe, asilimia 61 ya Wafaransa walisema Macron ndie aliye ibuka mshindi katika mjadala huo ambapo pia wanaweza kumchagua siku ya Jumapili.
Ameonyesha kwamba ana ufahamu mkubwa kuhusu uchumi, pili anajua ukweli na kama ni lazima anaweza kupambana vizuri hadi chini ya kiwango chake.
Marine Le Pen ameonyesha kuwa yeye ni binti ya baba yake anayependelea utawala wa mabavu vilevile ni malkia wa matusi. Yeyote anayependelea misemo ya kitaifa, ubaguzi, kuwatenga watu basi bila shaka atampa Marine Le Pen kura. Chama cha National Front si tu kuhusu kukielewa, lakini cham hicho kinatokana na imani kali.
Hakuna mjadala: si kwa wenye kuona mbali au walio wajanja zaidi watakaoweza kuishinda itikadi hiyo. Uwiano wa kihistoria ni kwamba si bahati mbaya au labda ajali kilichopo ni kwamba baadaye huko nchini Ufaransa hakuna mtu atakayeweza kusema kuwa hakulijua hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment