Generali Mkuu wa jeshi la Ujerumani amesema Alhamisi
(04.05.2017) bado haiko wazi iwapo afisa wa jeshi aliekamatwa wiki
iliopita kwa tuhuma za kupanga shambulio lilichochewa kibaguzi ni sehemu
ya mtandao mkubwa zaidi.
"Hatujuwi kwa wakati huu ..tunajaribu kuchunguza mazingira kuhusu
mtuhumiwa ." ametamka hayo Generali Volker Wieker mkuu wa majeshi ya
Ujerumani Bundeswher wakati akizungumza na kituo cha matangazo cha ARD.Vyombo vya habri vya Ujerumani vimeripoti kwamba maafisa wanaangalia uwezekano wa kuwepo kwa kundi la mtandao wa watu watano wenye kumhusu luteni alietajwa kwa jina la Franco A. mwenye umri wa miaka 28 aliekamatwa kwa tuhuma za kupanga shambulio la kibaguzi.
Wieker leo alikuwa anatarajiwa kukutana na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen mjini Berlin akiwa pamoja na magenerali wengine na maadimeri 100 kujadili kile waziri wa ulinzi alichokisema uongozi dhaifu jeshini.
Hapo jana Von der Leyen alitembelea kambi za kijeshi katika mji wa mpakani na Ufaransa wa Illkirch ambako ndiko alikukowepo Franco A. akitumika katika brigedia ya Ujerumani na Ufaransa ilioanzishwa mwaka 2010 kama mfano wa ushirikiano wa mipakani baina ya nchi hizo mbili.
Udhaifu wa uongozi
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursulavon der Leyen amesema "Nataka kuweka wazi kwamba sehemu kubwa ya wanajeshi nawaheshimu kikamilifu na sote tunaona fahari kwa ajili yao.
Ndio sababu nilisema wazi kabisa mwishoni mwa juma matukio kama yale yaliyotokea Pfullendorf, Bad Reichenhall,Sondershausen na Illkirch yanazusha masuali kuhusu tabia kama vile shahada ya uzamifu ilikuwa haikupaswa kupita na suala la uongozi. Na hivyo ndivyo taarifa yangu inavyosema."
Von der Leyen ameshutumu kushindwa kwa viongozi wa mwanajeshi huyo aliyekamatwa kwa tuhuma za kupanga shambulio la kibaguzi kuchukuwa hatua baada ya kuwasilisha tasnifu ya shahada ya azamili iliokuwa ikionyesha dhahir ubaguzi na ilikataliwa na chuo kikuu cha Ufaransa.
Wieker amesema mwaka huu ulianza kwa mfululizo wa mageuzi ya kimuundo jeshini baada ya kashfa ya dhila za ngono na maonevu katika kituo chake cha mafunzo ya operesheni maalum kusini mwa Ujerumani kulitinigisha jeshi hilo la ulinzi la Ujerumani.
Mwezi uliopita Von der Leyen alimtimuwa generali aliekuwa akisimamia mafunzo kukabiliana na matatizo yaliokuweko katika kituo hicho.
Hapo Jumanne waziri huyo alifuta safari yake ya Marekani na kuwaita maafisa wa ngazi ya juu jeshini kuzungumzia kashfa kadhaa zilizoikumba jeshi baada ya kukamatwa kwa mwanajeshi huyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment