Watu watano wamefariki dunia katika kijiji cha Ngiresi wilaya ya Arumeru
mkoani Arusha baada ya mti mkubwa kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala
usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kuanguka kwa mti huo kumetokana na
athari za mvua zinazoendela kunyesha.
Amesema kuwa waliofariki dunia ni watoto watatu ambao walikuwa wanafunzi
na vijana wa wiwili. Kamanda huyo amesema taarifa zaidi atatoa hapo
baadae.
SHARE
No comments:
Post a Comment