TRA

TRA

Thursday, June 29, 2017

Airtel mwendo mdundo Maonesho ya Sabasaba, yatoa ofa kabambe

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !






Meneja Uuhusiano wa Airtel,  Jackson Mmbando  (kulia)  na Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel,  Veronica Valentine (kushoto) wakionesha simu aina ya ZTE na Motorola katika banda la Airtel lililoko katika viwanja vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba, simu hizo zitauzwa kwa bei ya ofa ya shilingi 16,000 tu na mteja ataunganishwa na kufurushi cha muda wa maongezi kwa mwezi mzima cha shilingi 10,000 BURE. Katikati ni Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel, Tumwidike Michael
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imetangaza ofa kabambe wakati wote wa maonyesho ya biashara ya sabasaba mwaka huu zitakazowawezesha wateja wake na wale  wapya kuunganishwa na huduma za mtandao kwa gharama nafuu na pia kujipatia simu bomba kwa bei nafuu.

Akiongea na waandishi wa habari katika banda la Airtel lililopo viwanja vya sabasaba Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “dhamira yetu Airtel ni kuendelea kuunganisha jamii kwa bidhaa na huduma, hivyo kwa msimu huu maonesho ya saba saba tutatoa ofa nyingi sana ikiwemo  simu aina ya ZTE GS 500, Motorola C113, Motorola F3 na Motorola C117 kwa sh. 16,000 tu na  mteja akishanunua ataunganishwa na bando la sh. 10,000 litakalodumu kwa muda wa mwezi mmoja”

“Unaweza ukaona hapo gharama ya simu inakuwa nafuu na kisha  unaunganishwa na kifurushi cha mwezi mzima BURE kuongea na ndugu, jamaa, na marafiki huku ukifaidi huduma zingine za Airtel” alieleza Mmbando

Katika banda letu ndani ya saba saba mwaka huu pia huduma zitakazopatikana ni pamoja na   kubadilisha laini, huduma za Airtel Money, simu za smartphone za kisasa na origino, huduma ya Timiza Vicoba, kuelekezwa jinsi yakusoma masomo ya ufundi kwa njia ya simu VETA kupitia Vsomo pamoja na kujua jinsi yakufungua biashara ya Duka la Airtel popote na jinsi ya kupata faida yako”

Mmbando alisema kuwa “Airtel imekuwa ni desturi yetu kuleta huduma na bidhaa zetu katika maonyesho haya ya biashara kila mwaka na kukutana na wateja wetu ana kwa ana ili kutoa elimu zaidi kuhusu huduma zetu mpya na za kibunifu tunazozitoa kila mwaka”.

“Natoa wito kwa Watanzania kutembelea banda letu na kujipatia simu huduma za kimtandao zote kwa  gharama nafuu na vilevile kukutana na watoa huduma wetu na kupata elimu juu ya huduma mbalimbali  ikiwemo Kupata maelekezo ya kupata mikopo ya vikundi kupitia huduma ya Timiza vikoba.    Kupata maelekezo ya kuweza kufanya biashara za Airtel kokote Tanzania kupitia mfumo wa Maduka ya Airtel AMSHA pamoja na huduma nyingine nyingi” aliongeza Mmbando.
 

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger