
Akizungumza kwenye Clouds FM Juni 15, 2017 Alhaj Mzee Yusuph amegusia pia jinsi maneno ya watu yalivyofuata baada ya kutangaza na hatimaye kuacha kabisa muziki huku akielezea namna alivyokuwa anakataza watu kwenye Kundi lake wasitende maovu.
"Mimi nimeacha muziki kwa sababu nataka kuwa Muumuni wa Dini ya Kiislamu na kumfuata Mtume Muhammad (SAW). Nilipopata nafasi ya kwenda kuhiji Makka na kushika Al Kaaba nilimuomba Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu.
“Nilipoanza kubadilika nilikuwa nakataza pombe kwenye Band yangu. Siku nisiyowepo walikuwa wanasema Simba leo hayupo. Nilipokuwa nakataza haya mambo wengi walikuwa wakiniambia kwa nini nisifungue Madrasa. Kubadilika kwangu niliachana kwanza na starehe magoma kwanza maana ilikuwa ni kama kunywa maji tu unaposikia kiu.
SHARE
No comments:
Post a Comment