TRA

TRA

Tuesday, June 13, 2017

Alichoandika Fred Mpendazoe kuhusu kauli ya Rais Magufuli

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Alichoandika Fred Mpendazoe kuhusu kauli ya Rais Magufuli

Ninaona maandiko mengi yakieleza kwamba hatua nyingi zinazochukuliwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi mahiri wa JPM, yalisemwa na Chadema kupitia Tundu Lissu au Mnyika au Mbowe. Hii si hoja imara.

Hapa duniani wapo watu ambao wanaweza kusema jambo ukadhani wanasema jambo hilo kwa dhati kumbe wanaamini tofauti kabisa.

Mfano Chadema walimsema sana Lowassa kama fisadi kwa zaidi ya miaka 10, lakini hawakuyaamini waliyoyahubiri. Ndiyo maana mwaka 2015 wakampokea Lowassa kuwa mgombea urais. Watanzania wakaihukumu Chadema kwenye uchaguzi Mkuu.


Wabunge wa Chadema wamehubiri sana demokrasia na kufanya maandamano kudai demokrasia pana. Wabunge hao walifunga midomo kuonyesha hisia hizo wakiwa bungeni. 
Lakini uteuzi wa wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki ikadhihirisha kwamba wanachokisema si kile wanachokiamini. Ndani ya Chadema demokrasia ni kwa masilahi mapana ya kikundi cha watu.

Kwa hiyo madai ya Chadema na viongozi wa Chadema kudai kwamba yanayotekelezwa kwa sasa wao waliyasema siku nyingi ni hoja isiyo na mashiko.

Jambo lililo mhimu na la msingi ni mwenendo chanya wa viongozi na wanachama wa chama cha siasa kwa jamii. Pili chama cha siasa kinatakiwa kusimamia kinachokiamini. Siyo kuhubiri tu.

Kingine, lugha zinazotumika na baadhi ya viongozi wa Chadema mara nyingi huonyesha upungufu wa maadili na inawafanya watanzania wajiulize, je watu hawa wakipewa madaraka watakuwaje ? 

Rais JPM anafanya kazi njema, watanzania tumuunge mkono.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger