Watu walio na umri
wa zaidi ya miaka 75 ambao hutumia dawa aina ya Aspirin baada ya kupata
kiharusi au maradhi ya moyo wako hatarini kupata matatizo ya kuvuja damu
tumboni, Shirika la utafiti wa kitabibu Lancet limeeleza.
Lakini wamesisitiza kuwa Aspirin ina faida muhimu kama vile kuzuia maradhi ya moyo.
Utafiti wa kitabibu nchini Uingereza umeashiria kwamba kumeza vidonge vya dawa aina ya Aspirin kuna athari kubwa zaidi kuliko ilivyodhaniwa hapo awali hususan kwa watu wenye umri mkubwa.
Dawa hiyo ambayo inatumiwa kuzuia mshtuko wa moyo na maradhi ya kiharusi imehusishwa kwa siku nyingi kusababisha matatizo ya uvujaji wa damu ndani ya tumbo.
Wataalam hao wametahadharisha kuwa kusitisha ghafla matumizi ya Aspirin kunaweza kuleta madhara, hivyo mtu yeyote anashauriwa kupata ushauri wa Daktari ikiwa anatakiwa kubadili dawa.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment